
GARI LILILOPATA AJALI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP ENEO LA TANANGOZI -IRINGA
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA BWANA EZEKIEL MWAITELEKE
(MAREHEMU) MAJIRA YA SAA SITA NA NUSU MCHANA NA KUSABABISHA VIFO VYA
WATU WATANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO DESEMBA 4, 2012
![]() |
BAADHI
YA AKINA MAMA WASAMARIA WEMA WA TANANGOZI IRINGA WAKIJARIBU KUMPEPELEA
MMOJA WA MAJERUHI WA AJALI ILIYOTOKEA DESEMBA 4,2012 HUKO TANANGOZI IRINGA
LIKIHUSISHA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP LILILOINGIA NYUMA YA TRAILER T 566
BNQ AMBAPO WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWA WAKITOKEA DAR KWENDA MBEYA
WALIFARIKI PAPO HAPO
6:BAADHI YA WASAMARIA WEMA WAKITOA MOJA YA MAITI KUTOKA KATIKA GARI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA DESEMBA 4,2012 WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWEMO KATIKA GARI HILO WALIFARIKI PAPO HAPO(PICHA ZOTE NA MISANJO LIVIGHA (MLALAHOI ALWATAN WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM |

GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA
NA TRAILER NAMBA T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP
HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO
HAPO WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4

Ajali mbaya imetokea mkoani Iringa
mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu
wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani
mmoja.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku chanzo kikitajwa kuwa ni
kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa gari ndogo
marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa kulimudu na kulipalamia
lori kwa nyuma.
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha kwa mwendo kasi na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa gari hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.
Hivyo katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majina ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment