Serikali ya Libya imesema kuwa mtoto wa Kiongozi wa
zamani wa nchi hiyo, Saadi Gaddafi, ameondoshwa nchini Niger hivi sasa
anashikiliwa mjini Tripoli.
Saadi alitoroka baada ya baba yake, Kanali Muammar
Gaddafi kuuawa wakati wa mapinduzi yaliyofanyika mwaka 2011 nchini Libya.
Anashutumiwa kuwafyatulia risasi waandamanaji na anadaiwa
kutekeleza uhalifu mwingine wakati wa utawala wa baba yake, yeye alipokuwa
Kiongozi wa vikosi maalum vya kijeshi.
Serikali ya Libya imetoa taarifa hiyo mapema siku ya
alhamisi kuwa wamempokea akitokea Niger.
awali , Niger ilikataa ombi la Libya ilipotaka
imsafirishe Saadi, huku waziri wa sheria wa Niger akihofu kuwa Saadi
atahukumiwa adhabu ya kifo.
No comments:
Post a Comment