Kikosi
hicho kitapiga kambi katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena, lakini kitakuwa chini
ya usimamizi wa Nigeria.Nchi ya Chad, Cameroon, Niger na Benin pia zitatoa
wanajeshi wake.
Baada
ya mkutano huo uliofanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, katibu mkuu wa
wizara ya ulinzi ya Nigeria, Aliyu Ismail, amesema kikosi hicho kitakuwa tayari
kuanza kazi ifikapo mwezi July mwaka huu:"viongozi wa nchi na serikali za
nchi za ukanda wa ziwa Chad na Benin zimechukua uamuzi ufuatao.
kupitisha
dhana ya ufanyaji kazi, mikakati ya ufanyaji kazi na nyaraka zinazohusiana na
kuundwa kwa vikosi vya pamoja katika kupambana na kundi la kigaidi la
wapiganaji wa Boko Haram, kupitisha kupelekwa kwa vikosi hivyo katika makao
makuu ya Ndjamena, Chad, kwa utekelezaji wa rasilimali watu na mahitaji ya
kifedha.
Kwa hisani ya http://www.bbc.com/
No comments:
Post a Comment