“Usiku wa manane, kati ya saa saba na
saa nane hivi, Nilisikia vishindo vya nyayo vikitokea sebuleni ambako
mwanangu Shukuru na Edron walikuwa wamelala. Ghafla nikamwona mume wangu
ameshika upanga ananishambulia kichwani. Nikawa nashangaa na
kuwaangalia usoni bila kujua kwa nini alikuwa ananishambulia. Akasema,
“Nyamaza!”
Ofisa mmoja wa polisi alipendekeza nimwulize
Kulwa kama mabaki ya Maganga bado yapo kaburini kwa kuwa halikujengewa
kwa nondo na zege.
Nilimshauri awasilishe wazo lake kwa viongozi wake
ili waiombe Mahakama ruhusa ya kulifukua kaburi la Maganga na kupata
uhakika kama viungo vyake bado vipo au vimeondolewa.
Niliwaacha polisi wakiendelea na uchunguzi wao na mimi nikaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.
Niliwaacha polisi wakiendelea na uchunguzi wao na mimi nikaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.
Nilipokea taarifa za jaribio la kumdhuru mtoto wa
miezi saba ambaye ana ulemavu wa ngozi, Makunga Baraka Februari 5, mwaka
huu katika Kijiji cha Nyaruhande, Kitongoji cha Nyasubi, Kata ya
Nyaruhande, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu. Nilizungumza na mama mzazi
wa mtoto huyo, Jane Daudi ambaye aliniambia kuwa alikuwa amehifadhiwa
kwa muda katika kituo cha polisi kwa usalama wa mwanae.
“Nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha
kuwa ni George wa eneo la Ndiko. Akaniambia, “Dada nakuhurumia sana kwa
kuwa una mtoto mwenye ulemavu wa ngozi. Niliwasikia watu hotelini
wakipanga njama za kuja kumuua.” Niliogopa sana na nikamweleza mama
yangu. Tukaenda hadi kwa mwenyekiti wa mtaa hatukumkuta. Baadaye tukatoa
taarifa kwa wanakijiji.
Hawakutuamini. Hawakutaka kuja kutulinda. Kabla ya
saa tatu usiku watu watatu walikuja nyumbani kwetu na kuanza kuturushia
mawe dirishani na mlangoni. Wanakijiji wakawaona na wakawafukuza lakini
hawakuwakamata. Usiku ule wanakijiji walipeana zamu kutulinda.”
“Kesho yake asubuhi Mwenyekiti wa Mtaa
akaniandikia barua kwenda polisi na wanakijiji wakatusindikiza. Polisi
wanafuatilia taarifa nilizowapa. Naogopa sana. Nahofia maisha ya
mwanangu Makunga. Sitaondoka polisi hadi hapo nitakapopata ulinzi
mkali,” anasema Jane.
Maria Chambanenge (39)
Nilipokea taarifa nyingine za kushambuliwa kwa Maria Chamanenge (39) katika Kijiji cha Mkowe, Miangalua, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mkoa wa Rukwa.
Nilipokea taarifa nyingine za kushambuliwa kwa Maria Chamanenge (39) katika Kijiji cha Mkowe, Miangalua, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mkoa wa Rukwa.
Nilikwenda kumwona Maria katika Hospitali ya Mkoa
ya Sumbawanga. Kulikuwa na ulinzi mkali na tulielezwa kwamba tunapaswa
kupata kibali cha polisi ili kumtembelea wodini.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi alikuwa safarini kikazi. Maofisa tuliowakuta walituelekeza kuwa kibali kinapatikana kwa Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO).
Kamanda wa Mkoa wa Polisi alikuwa safarini kikazi. Maofisa tuliowakuta walituelekeza kuwa kibali kinapatikana kwa Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO).
Tulirejea tena hospitali na baadaye tulionana na
Kaimu Mganga Mkuu, alitupa idhini ya kuzungumza na Maria lakini chini ya
usimamizi.
Maria alikuwa bado ana maumivu makali, baada ya
kukatwa mkono wa kushoto. Madaktari walituhakikishia kwamba hali yake
inaendelea vizuri kwa upande wa matibabu. Swali lilikuwa je, kwa upande
wa kisaikolojia?
Maria ni albino na haoni vizuri. Sasa ameongezewa
ulemavu wa viungo. Huyu ni mama wa watoto wanne: Shukuru (8), Edron (6),
Rahab (3) na Emma (miezi mitano). Mama huyu ni mke wa tatu wa Gabriel
Yohana. Atawaleaje watoto wake akiwa na mkono mmoja sasa? Atafanyaje
kazi za nyumbani na za kilimo bila mkono wa pili?
Baada ya kumjulia hali, nilimwomba anielezee jinsi
alivyoshambuliwa na kukatwa mkono wa kushoto usiku wa Februari 11,
mwaka huu, chumbani akiwa amelala na wanae.
“Usiku wa manane, kati ya saa saba na saa nane hivi, Nilisikia vishindo vya nyayo vikitokea sebuleni ambako mwanangu Shukuru na Edron walikuwa wamelala. Ghafla nikamwona mume wangu ameshika upanga ananishambulia kichwani. Nikawa nashangaa na kuwaangalia usoni bila kujua kwa nini alikuwa ananishambulia. Akasema, “Nyamaza!” Mimi nikawa nalia. Akasema, Pole! Nyamaza!”
Source:Mwananchi

No comments:
Post a Comment