![]() |
Rais Mpya wa Venezuela Nicolas Maduro |
Tume ya uchaguzi nchini venezuela imetangaza
kiongozi wa kisoshalisti Nicolas Maduro kama mshindi wa uchaguzi wa
urais kwa asilimia 51 tu ya kura.
Hata hivyo ushindi huo dhidi ya mpinzani wake
mkuu Henrique Capriles ulikuwa ni wa chini ya asilimia mbili, ikiwa ni
chini ya robo ya kura zipatazo milioni 15 ya zile zilizopigwa .Ni ushindi mdogo zaidi ikilinganishwa na ule alioupata kiongozi wa chama chake hayati rais Hugo Chavez,mwaka jana, muda mfupi kabla ya kifo chake.
Kufuatia tangazo la ushindi huo Bwana Maduro alivaa mavazi yenye rangi za bendera ya Venezuela akidai uchaguzi wake ni wa haki na wa kisheria na akawataka raia wawe watulivu. Aliahidi kuendeleza sera za Bwana Chavez.
Pindi habari zilizpojitokeza kuwa Maduiro alikuwa mshindi, wafuasi wake walianza kusherehekea mjini Caracas, huku wafuasi wa upinzani nao wakianza kupiga sufuria kuonyesha ghadhabu zao.
Katika hotuba yake ya ushindi akiwa nje ya ikulu ya rais, bwana Maduro, aliambia wafuasi wake kuwa ushindi wake ni halali na umeambatana na sheria.
Aliongeza kuwa kuchaguliwa kwake kunaonyesha kuwa marehemu Hugo Chavez anaendelea kushinda vita vikuu.
Aliwataka wale waliompigia kura na wapinzani wake kushirikiana kwa niaba ya ya nchi nzima.
No comments:
Post a Comment