Madaktari nchini
Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya
kisayansi.
Walitumia mfano wa
seli ya uke na mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa
kuzingatia wastani na umbo la kila mwanamke.
Baada ya matibabu
hayo, wanawake hao wote inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na
kamilifu,matamanio, kuridhishwa wakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata
maumivu yoyote wakati wa tendo la ndoa.
Wataalamu walisema
kuwa utafiti wao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi
la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za
matibabu.
Wanawake hao
walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya
maumbile , tatizo linalojulikana kama ‘vaginal aplasia.’
Matibabu ya kisasa kwa
tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngozi au sehemu
ya utumbo inatumika.
Celi zilichukuliwa
kutoka kwa kizazi cha kila wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile
na kukuzwa katika maabara ili kuweza kuzaana.
Picha za kizazi cha
wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.
Hili bila shaka ni
jambo geni katika sayansi ya matibabu na pia inatoa taswira ya mambo
yatakavyokuwa katika siku za usoni.
Jambo la Kutumia celi
za mwili kubadilisha maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia
wagonjwa kupata kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo.
Sasa unaweza kuongeza
kwenye orodha hiyo, uke na pua.
Kwa hisani ya BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment