![]() |
Waziri Mkuu wa Mpito wa Ukraine |
Waziri Mkuu wa mpito wa Ukraine Arsenity Yatsenyuk amewaambia viongozi wa
eneo la mashariki mwa nchi hiyo kwamba amekusudia kuwaongezea madaraka zaidi
kwenye eneo hilo.
Hata
hivyo hajafafanua ni kwa kiasi gani atawapa mamlaka hayo na kwamba madaraka
hayo kama yanaweza kuwaridhisha wakazi wa eneo hilo lenye viwanda la Mashariki
mwa Ukraine ambalo linataka kujitenga.
Bwana
Yatsenyuk ameutembelea mji wa Donetsk katika jitihada zake za kushughulikia
msimamo wa waandamanaji wanaounga mkono Urusi ambao wameteka majengo ya
serikali za mtaa na kutangaza uhuru kutoka nchi ya Ukraine.
Wanaharakati
pia wameendelea kushikilia majengo ya serikali katika mji wa Luhansk.
Tayari
Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuchochea uvunjifu wa amani nchini Ukraine.
No comments:
Post a Comment