Umoja wa Mataifa umetuma onyo kali kwa Serikali ya
Burundi na kuitaka kuchukua hatua za haraka kushughulikia vurugu za kisiasa na
kuheshimu haki za binadamu. “Tuna imani kwamba serikali ya Burundi
itazingatia haraka iwezekanavyo na kushughulikia (matatizo yote) yanayosababisha
vurugu na ukiukwaji wa haki za bin adamu”, amesema msemaji wa Umoja wa
Matiafa Stéphane Dujarric.
Aidha, umoja huo umebainisha kuwa endapo vitendo vya ukiukwaji wa
haki za binadamu na uchochezi wa vurugu vitaendelea, basi wahusika watawajibika
mbele ya mahakama za kimataifa.
“iwapo hakutochukuliwa hatua, huku ukiukwaji wa haki za binadamu
zikiendelea, hatutosita kuwachukuklia hatua za kisheria wahusika, na
ikiwezekana wafikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa wajibu tuhuma
zinazowakabili”, ameendelea kusema Dujarric.
Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kitengo cha kuzuia mauaji
ya kimbari, Adama Dieng yuko ziarani mjini Bujumbura, ambako atajadili hofu hio
ya kutokea kwa mauaji ya kimbari na viongozi wa Burundi.
Onyo hilo ni miongoni mwa tahadhari ziliyokua zikitolewa hivi
karibuni na Umoja wa Mataifa pamoja na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa
Mataifa, Samantha Power.
Akiwa ziarani mjini Bujumbura hivi karibuni, balozi Samantha
Power, aliwatajka viogozi wa Burundi kuheshimu uhuru wa kisiasa, na vilevile
kuheshimu katiba ya nch, ambayo utawala unajaribu kuifanyiya marekebisho.
“ Tunasisitiza kuheshimu katiba ya nchi, ambayo ni sheria
mama ya Burundi, na vilevile kuheshimu haki za binadamu,” alisema Samantha
Power baada ya mazungumzo na rais Pierre Nkurunziza.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilielezea aprili mosi
wasiwasi wake, juu ya mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.
Katika tangazo liliyotolewa jana alhamisi, Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa, limeelezea kwa mara nyingine wasiwasi wake juu ya uhuru wa
kujieleza na mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa vya upinzani na mashirika
ya kiraia.
Wajumbe 15 wa baraza hilo, wameelezea wasiwasi wao juu “ya vitisho
na kufungwa kiholela pamoja na machafuko yanayotekelezwa na vijana kutoka vyama
vya kisiasa”.
Wajumbe hao wametoa wito kwa serikali ya Burundi kutowafumbia
macho wafuasi wa chama tawala ambao wamekua wakijihusisha na maovu mbalimbali,
mkiwemo unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa wiki kadhaa Umoja wa Mataifa umepata taarifa za kuaminika za
usambazaji wa silaha na sare za kijeshi kwa vijana wa chama tawala
Imbonerakure, shutuma ambazo zimetupiliwa mbali na serikali ya Burundi.
“Ni kweli kwamba kumekuwepo na matukio ya vurugu baina ya
vijana wa vyama mbalimbali vya kisiasa na sio tu chama tawala. Pia hakuna hali
ya kutokuwajibika kwa sababu uchunguzi unafanyika kuhusiana na matukio hayo na
tunapenda kuwaambia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa nchi ya Burundi
haisanbazi silaha kwa vijana wa chama hicho tawala”, naibu msemaji wa rais
wa Burundi, Willy Nyamitwe.
Burundi inapitia wakati huu mgogoro mkubwa wa kisiasa kutokana na
mgawanyiko kati ya chama cha rais Pirrea Nkurunzia, chenye wahutu wengi na
chama cha UPRONA, chenye watutsi wengi.
Bunge la Burundi lilikataa katikati ya mwezi wa machi kuidhinisha
mswada wa sheria ya kufanya marekebiho ya katiba, ambayo kwa mujibu wa upinzani
ingelisababisha taifa hilo kuingia katika dimbwi la machafuko ya kikabila kama
yale yaliyoshuhudiwa katika miaka ya 1993-2006.
Vyombo vya sheria vya Burundi viliwahukumu hivi karibuni kifungo
cha maisha jela wafuasi 21 wa chama cha upinzani cha MSD kwa kuwatuhumu kwamba
“walianzisha vurugu wakitumia silaha”, baada ya makabiliano na polisi ambayo
iliwakatila wasifanye mazowezi ya kukimbia, wakati vijana wa chama tawala
wamekua wakifanya mazoezi hayo kila jumamosi.
No comments:
Post a Comment