Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja
na kumi na tano wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya
kanisa kuporomoka nchini Nigeria.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao
wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea
kanisa hilo la 'All Nations in Lagos', ambalo linaongozwa na mhubiri T.B.
Joshua.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona
ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe
kuporomoka.
No comments:
Post a Comment