Raia wa Scotland wamefanya uamuzi wa mwisho kuwa wataendelea kubaki sehemu ya
Uingereza , raia kwa pamoja wamekataa uhuru wa Scotland.
Maeneo
31 kati ya 32 wamepika kura ya HAPANA siku ya Alhamisi na kuongoza kwa kura
1,914,187 dhidi ya 1,539,920.
Ushindi
huo ni asilimia 55 dhidi ya 45 waliokuwa wakiunga mkono hatua ya kujitenga.
Waziri
Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa
kura ya maoni.
No comments:
Post a Comment