Mahakama
ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemtaka raisi
wa Kenya Uhuru Kenyatta kufika
mahakamani tarehe 8 mwezi Oktoba licha ya majaji wanaotarajiwa kusikiliza kesi
dhidi yake kuiahirisha.
majaji katika mahakama hiyo wanataka
kumhoji juu ya madai kwamba serikali yake imeficha hati iliyoombwa na waendesha
mashitaka wanaosikiliza kesi yake ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Kesi hii imekuwa ikicheleweshwa mara
kadhaa sasa.hata hivyo raisi kenyata amekanusha kuandaa mauaji ya kikabila
baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Takribani watu elfu moja mia mbili
waliuawa na laki sita kuyakimbia makazi yao.
Wiki mbili zilizopita, waendesha
mashitaka waliomba kesi dhidi yake kuahirishwa kwa muda usiojulikana, kwa vile
hawakuwa na ushahidi wa kutosha kwa sababu ya serikali ya Kenya kuweka vizuizi.
No comments:
Post a Comment