Friday, September 19, 2014

SAA ZA GHARAMA ZAWAPONZA MAOFISA WA FIFA



Shirikisho la soka la dunia FIFA, limewaambia viongozi wanaounda kamati ya utendaji na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo kurejesha saa zipatazo 65 za gharama walizopokea kama zawadi kipindi cha kuelekea kombe la dunia huko Brazil mwaka huu.
FIFA imesema kitendo cha kurejesha saa hizo ni kutunza nidhamu.
Saa hizo zinakadiriwa kuwa na gharama ya dolla elfu ishirini na tano kila moja na zinatakiwa ziudishwe Octoba 24 ,mwaka huu.
Saa hizo za kumbukumbu ya Parmigiani ziligawiwa na shirikisho la soka la Brazili (CBF) wakati wa mkutano wa maandalizi wa FIFA uliofanyika mjini Sao Paulo.
FIFA imesema kuwa kanuni za maadili zinazuia viongozi kupokea zawadi ambazo zinathamani zaidi au zenye kuonesha ishara fulani.

Inasemekana kwamba saa hizo zitatolewa kwa taasisi zinazojitegemea na si sile zinazojali maslahi huko Brazili.

No comments:

Post a Comment