Polisi walipoitwa
mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu
wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo
mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya
wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu
zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa
kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi
pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na
simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.
Kila
wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu
na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka
hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo
sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema
mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji
mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama
ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia
kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata
staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700
sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya
binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa
za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu,
lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.
Kwa hisani ya BBC-Swahili
No comments:
Post a Comment