Wanajeshi
wana matumaini ya kuwakamata wanajeshi waasi ambao waliongoza mapinduzi ya wiki
hii katika jaribio la kumpindua rais Pierre Nkurunziza.
Nkurunziza
ametaka kusitishwa kwa maandamano hayo na kuyahusisha na jaribio hilo la
mapinduzi.
Lakini
baadhi ya makundi ya waandamanaji yamekana madai hayo na kumtaka tena rais
kuiheshimu katiba.
Marekani
nayo inasema kuwa Nkurunziza hastahili kuwania muhula mwingine ikiongeza kuwa
serikali yake itawajibika kwa chochote kile kitakachotokea.
Kwa hisani ya BBC-Swahili
No comments:
Post a Comment