Wednesday, November 2, 2016
RAISI MAGUFULI AWASILI KUTOKA ZIARA YA NCHINI KENYA
Rais Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya.
- Alikuwa nchini Kenya katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili
Mh.Raisi akisalimiana na viongozi wa juu Serikalini mara baada ya kutua
Wednesday, October 19, 2016
KUTOKA KWA MDAU WETU GUNDA FOUNDATION

Mwaka 2016 Shirika la Twaweza Afrika Mashariki lilizindua utafiti wake (http://twaweza.org/go/uwezo-tz-2014) uliofanyika mwaka 2015 ukionesha ongezeko kubwa la watoto kushindwa kusoma ilhali wapo madarasa ya juu mfano darasa la nne nakuendelea.
Tafiti hizi sio za kusoma na kuangalia hivi hivi. Kila mmoja wetu anayo nafasi ya kusaidia anguko hili ambalo linazidi kumomonyoa na kuifanya Elimu kwa watoto wetu kuwa duni na yakukatisha tamaa.
Kama Marafiki wa Elimu kupitia Gunda Foundation Tanzania, tumekua tukifanya Harakati mbalimbali za kuwasaidia watoto kupenda kujifunza na kujisomea vitabu ili kukuza maarifa na kuboresha maendeleo ya ufahamu walionao.
Mwaka 2014 Gunda Foundation ilifanya Jitihada za mwanzo katika kuwasaidia watoto wa kata ya Msambara, Wilaya ya Kasulu mkoani kigoma kuweza kusoma.
Katika mradi huo ulijumuisha shule 7 za kata hio na jumla ya watoto 197 wa shule tano za kata hio waliingia katika utaratibu huu wakati wa likizo ya mwezi wa 12, 2014.
Watoto hawa walikua katika hatua tofauti tofauti za usomaji. Mbinu mbalimbali zilitumika ili kutambua uwezo halisi wa mtoto katika kusoma.
Utaratibu wa kuwatambua na kuwatenga watoto hawa ulikua kama ifuatavyo;
- Viliandikwa vikaratasi vikiwa na neno moja mpaka maneno mawili, kisha kutupwa katika eneo la shule vikiwa vya idadi ya kutosha;
- Wanafunzi wakiwa darasani waliruhusiwa kutoka darasani na kila mmoja alitakiwa aokote karatasi lolote atakalo liona katika mazingira ya shule yake na akisha okota basi akimbie mpaka katika uwanja wa shule na kusimama umbali wa mita 20 mbali na mwenzake;

- Bila watoto kusomeana vikaratasi hivyo kutokana na umbali waliosimama mmoja hadi mwingine, Mwalimu alianza kuita mwanafunzi mmoja baada ya mwingine na akifika mwalimu humuomba mwanafunzi amsomee neno lililoandikwa katika karatasi aliyoiokota.
- Kwa njia hii makundi kadhaa yalitenganishwa kulingana na uwezo wa mtoto kusoma neno hilo kwa vigezo vya bila kusita;
- Watoto walioonesha udhaifu mkubwa waliingizwa darasani na kuandikiwa silabi “a” mpaka “z” ubaoni na walitakiwa wasome silabi zote mmoja baada ya mwingine ili mwalimu ajiridhishe zaidi katika uwezo wa mwanafunzi kusoma;

- Hii ilifanyika ili kusaidia kumpa mtoto mkakati maalumu utakaomsaidia kusoma vizuri.
- Baada ya kuapata makundi ya uwezo tofauti wa usomaji mwalimu alianza mafunzo ya kuwaelekeza watoto kujifunza kusoma na programu hii ni ya mwezi mmoja na hufanyika katika kipindi cha likizo ya mihula ya wanafunzi.
Kumbuka: Ukihitaji kuona video ya vitendo hivi au matokeo wasiliana nasi kwa namba 0674 14 12 09 au Baruapepe: gmpollo@gmail.comau fika Chuo cha Ualimu Korogwe onana na Mwalimu Gunda.
Kuanzia mwaka huu 2016, Mwezi Octoba Marafiki wa Elimu kwa ushirikiano na Gunda Foundation wanatarajia kuifanya programu hii katika mkoa wa Tanga hususani katika Wilaya za Handeni Vijijini na Korogwe.
Kwa Korogwe pia itahusisha Darasa la watu wazima na wale waliokosa nafasi ya kujiunga na darasa la kwanza wakiwa na umri mkubwa ili kuwapa fursa ya kujua kusoma na kuandika.
Hivyo ukiwa kama mdau wa Elimu unaomba kama una mtoto, ndugu au jamaa asiejua kusoma na kuandika basi wasiliana nasi ili aweze kusaidiwa na HAKUNA MALIPO YOYOTE ATAKAYOCHANGIA KATIKA UJIFUNZAJI WAKE!

Sote tunawajibu kuwasaidia Watoto Wajifunze
Friday, August 5, 2016
Monday, July 18, 2016
Thursday, July 14, 2016
Tuesday, July 12, 2016
Mtoto apandikizwa pua mpya India
Madaktari nchini India wamepandikiza
pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la
uso.
Pua
ya Arun Patel iliharibika alipougua ugonjwa wa homa ya kichomi
Maambukizi
hayo yaliharibu pua yake akiwa mtoto mdogo.
Upandikizaji
kama huo ulifanywa nchini China mwaka 2013 ambapo mtu mmoja ambaye aliharibu
pua yake katika ajali alipewa pua mpya.
Wazazi
wa Arun walimchukua na kumpeleka katika daktari mwengine katika kijiji cha
jimbo la kati la Madhya Pradesh ambapo aliugua kichomi mda mfupi baada ya kuzaliwa.
Miaka
kadhaa baadaye,kundi moja la madaktari katika mji wa Indore liliamua kufanya
upasuaji usiokuwa wa kawaida ambapo Arun alipata pua mpya.
Mabaki ya Wafilisti yapatikana Israel
Watafiti wa mambo ya kale nchini Israel wamegundua makaburi ya kwanza ya
Wafilisti.
Makaburi hayo,
yaliyopatikana eneo la Ashkelon, yaligunduliwa mwaka 2013, lakini habari hizo
zilifichuliwa Jumapili.
Habari hizi ziliwekwa
siri muda huo wote kuzuia kushambuliwa na waandamanaji wa makundi ya Wayahudi
wahafidhina ambao hawakutaka makaburi hayo yafukuliwe.
Mafanikio
hayo yalitokea mwisho wa mwaka wa 30 wa uchimbaji ulioongozwa na kundi la Leon
Levy Expedition.
Viongozi
wa uchimbaji huo wanasema walipata makaburi yaliyozingirwa na manukato,
vyakula, mapambo, vito na silaha.
Yanadaiwa
kujengwa na kutumiwa kati ya karne ya 11 na karne ya 8 kabla ya kuzaliwa kwa
Yesu.
“Kwa
ugunduzi huu, tunakaribia kubaini siri za asili yao.”
![]() |
| Profesa Lawrence E. Stager ni mmoja wa wanaoongoza utafiti huo |
Wanaakiolojia
hao sasa wanafanya uchunguzi wa DNA pamoja na uchunguzi wa miale ya ukaa
kubaini watu hao waliishi wakati gani.
Wafilisti
huoneshwa katika Biblia kama maadui wakuu wa Waisraeli, na inadhaniwa walihamia
Israel kutoka maeneo ya Magharibi karne ya 12 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.
Anayefahamika zaidi
ni Goliath, mpiganaji ‘jitu’ ambaye kwa mujibu wa Biblia, aliuawa na Daudi
kabla yake kuwa Mfalme wa Waisraeli.
Katika
Biblia, wanaoneshwa kama watu wakatili lakini mabaki yaliyopatikana yanaonekana
kuashiria kwamba walikuwa na ustaarabu fulani.
Habari kwa hisani ya BBCSwahili
Saturday, July 2, 2016
AZAM MARINE WAJA NA SEA TAX
Kampuni ya usafirishaji majini ya Azaam Marine imekuja na huduma mpya ya usafirishaji wa majini jijini Dar es salaam.
UJENZI WA DARAJA LA KONGOWE - KIGAMBONI WAENDELEA
Daraja linalounganisha maeneo ya Mbagala Kongowe na Kigamboni lililopo eneo la Mbagala Kongowe ambalo lilikuwa shida kupitika wakati wa mvua kubwa sasa linajeungwa upya.Daraja hili ni kiungo kikukwa sana kwa wakazi waishio maeno ya Toangoma,Kibada na Kigamboni Kutokea Mbagala Kongowe.
Friday, July 1, 2016
KUTOKA BUNGENI
Kutoka Bungeni jijini Dodoma ,Wabunge wa kambi rasmi ya Upinzani jana asubuhi waliingia Bungeni wakiwa wote wamevalia nguo nyeusi walipohudhuria kikao cha Bunge la Bajeti.Baada ya Naibu Spika Dk Tulia Ackson kuingia Bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge walianza kunyanyua mabango mbalimbali na kutoka nje
Thursday, June 30, 2016
Wednesday, June 29, 2016
Thursday, April 21, 2016
Wednesday, April 20, 2016
RAIS MH.JOHN MAGUFULI AZINDUA DARAJA LA KIGAMBONI KATIKA PICHA
![]() |
| Raisi Mh John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi na wageni waliofika kushuhudia uzinduzi huo wa kihistoria wa daraja la kigamboni ambalo Mh Rais alishauri liitwe daraja la Nyerere |
![]() |
| Mh Raisi akikata utepe kuashiria ufunguzi wa daraja hilo |
![]() |
| Muonekano wa Daraja la Kigamboni |
Picha zote kwa hisani ya blog.ikulu.go.tz/
Tuesday, April 19, 2016
Monday, April 18, 2016
Saturday, April 16, 2016
Thursday, March 10, 2016
Wednesday, March 9, 2016
AJALI MAENEO YA MATUMBI
Alfajiri ya leo tar 9.3.2016,imetikea ajali maeneo ya matumbi Tabata ikihusisha daladala aina ya DCM lilikuwa likitokea Gongo la Mboto kuelekea Ubungo na maroli mawili moja la mizigo na jingine lilibeba ng'ombe.Idadi kubwa ya abiria walipoteza maisha .
Picha nyingine ni mbaya sana,samahani kwa hilo
Picha nyingine ni mbaya sana,samahani kwa hilo
Wednesday, December 23, 2015
Saturday, December 19, 2015
Friday, December 18, 2015
Thursday, December 17, 2015
Wednesday, December 16, 2015
WAZIRI ATOA SIKU 14 KUKAGUA MIKATABA YA AJIRA
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,Uratibu na Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu,Jenista Mhagama metoa siku 14 kwa maofisa kazi wote nchini,kukagua mikataba ya ajira nchini.
Waziri alitoa agizo hilo jana jijini Dar es salaam alipotembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha Tooku Tanzania Germent kilichopo Mabibo External,ambacho wafanyakazi wake wana mgogoro na Mwajiri wao wakiomba kuongezwa mishahara
Waziri alitoa agizo hilo jana jijini Dar es salaam alipotembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha Tooku Tanzania Germent kilichopo Mabibo External,ambacho wafanyakazi wake wana mgogoro na Mwajiri wao wakiomba kuongezwa mishahara
Subscribe to:
Posts (Atom)

















































