Shigongo akishirikiana na Mbunge wa Busanda-CCM,
Lolesia Bukwimba licha ya kukutanisha makundi yanayosigana pia waliandaa
mashindano ya soka ili kuhamasisha amani katika eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Shigongo alisema
kuwa wamefikia hatua kubwa katika utatuzi wao kwani viongozi wa dini
hizo walifikia mwafaka na kusaini mkataba wa amani.
Katika vikao hivyo ambavyo viliwashirikisha Mbunge Bukwimba na viongozi wa Serikali Wilaya ya Geita, Mchungaji Isaya Ikiri na Sheikh Ismail Ibrahim waliwekeana saini ya makubaliano ya amani.
Katika vikao hivyo ambavyo viliwashirikisha Mbunge Bukwimba na viongozi wa Serikali Wilaya ya Geita, Mchungaji Isaya Ikiri na Sheikh Ismail Ibrahim waliwekeana saini ya makubaliano ya amani.
Shigongo alisema kuwa kati ya makubaliano
waliyofikia pande hizo mbili ni kuwa Waislamu kuendelea kuchinja, lakini
Wakristo wanaweza kuchinja lakini nyama yao isiingie katika biashara ya
bucha.
“Pia pande zote mbili zimetakiwa kuwa makini,
kwamba atakayekiuka makubaliano hayo kachukuliwe hatua za kisheria kama
mtu binafsi na sio dini ihusishwe,” aliongeza Shigongo.sio dini Sheikh
Ibrahim, ambaye yuko katika msikiti wa Katoro, aliithibitishia gazeti
hili juu ya mwafaka huo
No comments:
Post a Comment