Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa
Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo
Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez
ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa
anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa
mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali
ya kijeshi kuendelea kupokea matibau. Hata hivyo maelezo zaidi
hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu
Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa
kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.Bwana Chavez amekua uongozini nchini Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini
No comments:
Post a Comment