Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo
kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya
wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na
kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Hata hivyo tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano asubuhi saa za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment