Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Asasi isiyokuwa
ya Kiserikali ya Human Settlements of Tanzania (Huseta), yamepangwa
kufanyika Jumatano na yataanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia nje
ya Ubalozi wa Uingereza hapa nchini.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi katika Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hajapata barua ya
kuomba kufanyika kwa maandamano hayo. “Lakini nitaangalia maudhui, kama
yanafanana na maandamano husika,” alisema.
Alisema akifika ofisini leo na kuiona barua ya
kuomba kufanyika, maandamano hayo atakuwa katika nafasi nzuri ya
kuzungumzia maandamano hayo.
“Nikipata barua ya maandamano hayo na kuona
maudhui yake, nitakuwa katika nafasi ya ama kuyaruhusu au
kutoyaruhusu,"alisema Kova
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Mwenyekiti wa Huseta, Dagan Kimbwereza, alisema Muingereza
huyo (jina linahifadhiwa) amekuwa akitumia mitandao ya kijamii, kuwashfu
Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mzengo Pinda.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa raia huyo wa
Uingereza bila ya kuwa na vithibitisho wa kile anachokisema, amekuwa
akikashfu mihimili mingine ikiwamo mahakama,tasnia ya habari na wananchi
kwa jumla.
“Baada ya kufika ubalozini wawakilishi wawili
watawasilisha azimio lenye saini za Watanzania wakiitaka Serikali ya
Uingereza kutoa tamko hadharani kwamba yenyewe haihusiki wala haisaidii
dharau na maovu mengine yanayofanywa na raia wake dhidi ya Taifa la
Tanzania,”alisema Kimbwereza.
Kimbwereza akionyesha kwa waandishi moja ya chapisho ambalo mtuhumiwa ameandika katika mitandao ya jamii ni ile inayosema;
Kikwete aitaka PCCB (Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa) kupambana na rushwa hadi katika Baraza la
mawaziri,’kundi moja la majambazi linaliambia kundi jingine la majambazi
kukamata mwizi” .
“Mahakama za Tanzania zimejaa rushwa na hazina
uwezo. Rais ndiye msimamizi wa katiba na yeye ndiye mhusika mkuu wa
ukiukwaji wa sheria” inasomeka moja ya hoja alizoziandika Sarah katika
mitandao ya kijamii. #
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment