![]() |
mmoja wa majeruhi |
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema
kuwa watu 10, wakiwemo maafisa wa polisi wawili, wameuawa mjini
Mombasa, Pwani ya Kenya. Tukio hilo lilitokea alfajiri, kuamkia leo
wakenya wanapopiga kura.
Hata hivyo polisi walithibitisha vifo vya
maafisa wao wawili vilivyotokea wakati polisi walipowapiga risasi
washambulizi waliokuwa wamejihami kwa mapanga. Lilikuwa shambulizi la
kulipiza kisasi.Washambulizi hao wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Pwani.
Mwandishi wa BBC, Karen Allen, anasema polisi waliweza kuthibitisha vifo vya wanne katika eneo la Changamwe, naye Hassan Majid aliona mtu mmoja kauawa eneo la Mishomoroni. Mwtu mwingine Moja ya miili hiyo ilikuwa imekatwakatwa.
Zaidi ya watu 1,000 waliuawa miaka mitano iliyopita katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Source:BBC
No comments:
Post a Comment