![]() |
Rais wa Syria Bashir al Assad |
Rais wa Syria Bashar al Assad amesisitiza kuwa hatajiuzulu kabla ya
mwisho wa kipindi chake madaraka mwaka 2014, wakati bomu lililotegwa
katika gari liua watu watatu katika mji mkuu Damascus.
"Kujiuzulu ni sawa na kukimbia", Assad amesema katika mahojiano na
gazeti moja la Argentina la Clarin wakati alipoulizwa iwapo anaweza
kufikiria kujiuzulu kama waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John
Kerry anavyotaka."Sifahamu iwapo Kerry ama yeyote mwingine amepata madaraka ya watu wa Syria kuzungumzia kwa niaba yao juu ya nani anapaswa kuondoka madarakani na nani anapaswa kubaki. Suala hilo litaamuliwa na watu wa Syria katika uchaguzi wa rais mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment