Akisoma bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu ripoti ya awali ya Tume ya kuchunguza kushuka kwa matokeo ,waziri wa Uratibu na Bunge Williamu Lukuvi amesema hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Baraza la Mawaziri ambao waliopokea taarifa ya tume hiyo ambayo imependekeza hatua hiyo.
Kwa mujibu
wa Tume hiyo, imependekeza mtihani wa kidato cha nne kusahihishwa upya
huku ikiyafuta yale yaliyotangazwa kwa ajili ya kuweka usahihi na njia
ya kuelekea kilele cha ubora wa elimu ya Watanzania wote.
Akizungumza
Bungeni leo mjini Dodoma, Lukuvi alisema kuwa mitihani hiyo inapaswa
kusahihishwa kwa kufuata kanuni ya mwaka 2011, hivyo uamuzi huo
umetolewa na Tume ya Waziri Mkuu Pinda aliyounda baada ya Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza matokeo ya kidato cha nne huku
asilimia 60 ya wanafunzi wote kufeli.
Suala hilo
liliibua mtafaruku mkubwa kwa wadau na wanasiasa wa Tanzania, wakililia
haki ya mtoto wa Tanzania kusoma, huku wakisema kufeli kwao kutaongeza
joto la maisha magumu kwa watoto hao ambao wengi wanatoka kwenye familia
masikini.
No comments:
Post a Comment