Kwa siku ya nane ya mazungumzo kati ya Kundi la nchi 6 zenye nguvu
duniani na Iran katika mji wa Lausanne Alhamisi jioni Aprili 2, makubaliano
kati ya pande mbili hatimaye yamefikiwa.
Iran na serikali za Magharibi wamesema "vigezo
muhimu" kwa "mfumo wa makubaliano" au "hatua" hatimaye
zimepigwa.
"vigezo muhimu" kwa mfumo wa makubaliano kuhusu
mpango wa Nyuklia wa Iran vimepatikana, ametangaza mkuu wa sera za nje wa Umoja
wa Ulaya, Federica Mogherini, katika mkutano na vyombo vya habari, akiwa pamoja
na mwenziye wa Iran katika mji wa Lausanne. Maneno haya yametumiwa na upande wa
Iran pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Umoja wa Ulaya na Marekani watasitisha vikwazo vyote vya
kiuchumi na kifedha vinavyohusiana na nyuklia. " Tuko mbioni sasa
kuandika rasimu ya Nakala ya mpango wa utekelezaji wa pamoja, ikiwa ni pamoja
na maelezo ya kiufundi katika wiki na miezi ijayo", amesema Federica.
|
Ni kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo Rais wa Iran
Hassan Rouhani akifuatiwa na viongozi kadhaa wa nchi za Magharibi wametoa
taarifa kwamba makubaliano kuhusu masuala nyeti ya mpango wa nyuklia wa Iran
yamepatiwa ufumbuzi. Zoezi la kuandika makubaliano ya mwisho linaweza kuanza
mara moja, kwa mujibu wa Hassan Rouhani. Mkataba wa mwisho unaweza kutiliwa
saini " Juni 30", Iran imethibitisha.
Makubaliano haya ya msingi yanaeleza kwamba theluthi mbili
ya uwezo wa sasa wa Iran wakurutubisha uranium usitishwe na kufuatiliwa kwa
kipindi cha miaka kumi, kwa mujibu wa chanzo cha Magharibi. vituo 6000 kwa
jumla ya 19000 vinavyorutubisha uranium vitafuatiliwa, vyombo vya habari vya
Iran vimethibitisha. " Uwezo wa kuipa thamani ya juu uranium
kutoka Iran utapunguzwa", amesema Federica Mogherini.
No comments:
Post a Comment