Joto la kisiasa limeendelea kupanda nchini Burundi kufuatia
nia ya rais Pierre Nkurunziza ya kugombea muhula wa tatu, huku wafanyakazi wa
serikali wanaopinga kugombea kwa Pierre Nkurunziza muhula wa tatu wakifutwa kazi.
Wakati
huohuo, Spika wa Bunge nchini Burundi, Pie Ntavyohanyuma amezuiliwa Alhamisi
wiki hii kusafiri kwenda nchini ubelgiji katika ziara ya kikazi. Wizara ya
fedha imemuomba kiongozi huyo kutoa maelezo kuhusu matumizi ya Euro elfu
thelathini aliyopewa alipofanya ziara ya kikazi nchini Kenya. Lakini wengi
wanaona kwamba kuzuiliwa kwa Spika huyo, kunaambatana na malumbano yanayojiri
wakati huu katika chama madarakani Cndd-Fdd.
Aliyekuwa
kiongozi wa chama cha Cndd-Fdd, Hussein Radjabu ameikosoa nia ya rais
Nkurunziza ya kutaka kugombea muhula watatu, akisema kwamba iwapo rais huyo
atafanya hivyo atakua amewakosea wafuasi wa chama cha Cndd-Fdd pamoja na raia
wa Burundi kwa ujumla.
Hayo
yakijiri, wito uliyotolewa na mashirika ya kiraia wa kuwataka raia popote pale
walipo kupiga honi, firimbi na kogonganisha vyuma saa sita mchana Alhamisi
Aprili 2, umeitikiwa mjini Bujumbura na katika sehemu mbalimbali za nchi.
Jumatano
wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari kiongozi wa muungano wa
mashirika ya kiraia Forsc, Vital Nshimirimana, amesema wito huo kwa raia ni
kama kadi nyekundu anayopewa mchezaji wa soka aliyefanya madhambi, akibaini
kwamba rais Nkurunziza atakua amepewa kadi nyekundu.
Hayo
yanajiri wakati Kaskazini mwa nchi hiyo, hasa katika mkoa wa Kirundo zaidi ya
raia 300 wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda, wakisema wanahofia usalama wao
kutokana na hali inayojiri wakati huu nchini mwao. Waziri wa Rwanda mwenye
dhamana ya wakimbizi, Serafine Mukantabana amesema serikali yake imejenga kambi
mbili ambapo watapewa hifadhi wakimbizi hao.
Waziri
Mukantabana ameongeza kuwa wako mbioni kuwapatishia matibabu baadhi ya
wakimbizi ambao wameanza kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment