Viongozi wa nchi za Ulaya
wanakutana leo Alhamisi mjini Brussels, nchini Ubelgiji kuzungumzia tatizo la
wahamiaji haramu wanaopitia katika bahari ya Mediterranean kwa kuingi Ulaya
wakitokea pwani ya Libya.
Safari za wahamiaji hawa zimekua
zikikumbwa na majanga hadi kusababisha vifo. Hivi karibuni wahamiaji zaidi ya
800 walifariki ndani ya majuma yasiyozidi mawili baada ya boti walizokuwemo
kuzama maji katika bahari ya Mediterranean wakielekea Ulaya wakitokea katika
pwani ya Libya.
Wakati
ambapo matukio hayo ya kuzama kwa boti zinazowasafirisha wahamiaji haramu
barani Ulaya yakiongezeka, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali
hivi karibuni vilitoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuchukua hatua zinazojitajiaka.
Jumatatu
Aprili 20 mawaziri wa mambo ya nje wa nchi ishirini na nane za Ulaya walikutana
mjini Luxembourg ili kujadili uwezekano wa kudhibiti hali hiyo.
Katika
mpango wa kukabiliana na uhamiaji haramu uliyoandaliwa mjini Luxembourg
Jumatatu wiki hii, kwanza kuna hatua ya kuzuia, inayounga mkono masuala ya
upelelezi.
Taasisi za
Europol na Eurojusts, polisi na majaji, pamoja na maafisa wa uhamiaji
wanaoteuliwa kwenye balozi za umoja wa Ulaya katika nchi wanakotoka wahamiaji
pamoja na nchi zinazowapokea, watakua wakitahmini kila siku orodha ya watu
wanaosafiri kuelekea Ulaya wakipitia majini au nchi kavu.
Halafu kuna
hatua ya kidiplomasia katika nchi zinazowapokea wahamiaji, hasa nchi ambazo
zinazopakana na Libya, ambayo imekua sehemu ya mapokezi kwa wahamiaji
wanaokimbilia Ulaya, kuchangia kudhibiti wimbi hilo la wahamiaji na kupunguza
ajali za majini.
Halafu pia
kuna kuzidisha mara dufu uwezo wa kifedha na meli kwa kazi ya uokozi na ulinzi
wa mipaka inayoingia barani Ulaya. Meli hizi zinaweza kuingilia kati mahali
popote katika maji ya kimataifa.
Hata hivyo
bado kuna hatua zingine ambazo zitajadiliwa kataika mkutano mwingine wa Umoja
wa Ulaya unaotazamiwa kufayika leo Alhamisi.
Hayo ya
kijiri, takwimu zinazotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) zinabaini kwamba
watu 800 walikufa maji katika ajali ya boti iliyotokea usiku wa Jumamosi
kuamkia Jumapili Aprili 19, baada ya boti waliyokuwemo kuzama katika bahari ya
Mediterranean. Boti hilo lilikua lilibeba mamia ya wahamiaji. Takwimu hizi
zimetolewa kulingana na ushahidi uliyotolewa na manusura 28 kila waliowasili
Catania, Sicily.
No comments:
Post a Comment