Friday, April 24, 2015
Thursday, April 23, 2015
WAKIMBIZI AZIDI KUMIMINIKA NCHINI RWANDA
Kambi ya Gashora nchini Rwanda inazidi
kupokea wakimbizi wanaotoka mkoa wa Kirundo nchini Burundi ,wengi wanakimbia
nchini mwao kutokana na usalama wa nchi
hiyo,wakimbizi hao wanatoka mikoa mbalimbai ya Burundi,vijana wa chama tawala inasemekana
kuwa wanahatarisha usalama wa nchi.Ujenzi wa mahema kwenye kambi hiyo
unaendelea,ila wakambizi wanalalamikia kuwa chakula hakitoshi.Wasimamizi wa
wakambizi wa nchi ya Rwanda wanasema kambi ni ya Muda tu ,Serikaliinafanya
mpango wa kuwahamisha na kuwapeleka Kirehe.inasadikiwa idadi ya wakimbizi imefikia
10000.
Mkutano wa EU kuangazia tatizo la wahamiaji
Viongozi wa nchi za Ulaya
wanakutana leo Alhamisi mjini Brussels, nchini Ubelgiji kuzungumzia tatizo la
wahamiaji haramu wanaopitia katika bahari ya Mediterranean kwa kuingi Ulaya
wakitokea pwani ya Libya.
Safari za wahamiaji hawa zimekua
zikikumbwa na majanga hadi kusababisha vifo. Hivi karibuni wahamiaji zaidi ya
800 walifariki ndani ya majuma yasiyozidi mawili baada ya boti walizokuwemo
kuzama maji katika bahari ya Mediterranean wakielekea Ulaya wakitokea katika
pwani ya Libya.
Wakati
ambapo matukio hayo ya kuzama kwa boti zinazowasafirisha wahamiaji haramu
barani Ulaya yakiongezeka, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali
hivi karibuni vilitoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuchukua hatua zinazojitajiaka.
Jumatatu
Aprili 20 mawaziri wa mambo ya nje wa nchi ishirini na nane za Ulaya walikutana
mjini Luxembourg ili kujadili uwezekano wa kudhibiti hali hiyo.
Katika
mpango wa kukabiliana na uhamiaji haramu uliyoandaliwa mjini Luxembourg
Jumatatu wiki hii, kwanza kuna hatua ya kuzuia, inayounga mkono masuala ya
upelelezi.
Taasisi za
Europol na Eurojusts, polisi na majaji, pamoja na maafisa wa uhamiaji
wanaoteuliwa kwenye balozi za umoja wa Ulaya katika nchi wanakotoka wahamiaji
pamoja na nchi zinazowapokea, watakua wakitahmini kila siku orodha ya watu
wanaosafiri kuelekea Ulaya wakipitia majini au nchi kavu.
Halafu kuna
hatua ya kidiplomasia katika nchi zinazowapokea wahamiaji, hasa nchi ambazo
zinazopakana na Libya, ambayo imekua sehemu ya mapokezi kwa wahamiaji
wanaokimbilia Ulaya, kuchangia kudhibiti wimbi hilo la wahamiaji na kupunguza
ajali za majini.
Halafu pia
kuna kuzidisha mara dufu uwezo wa kifedha na meli kwa kazi ya uokozi na ulinzi
wa mipaka inayoingia barani Ulaya. Meli hizi zinaweza kuingilia kati mahali
popote katika maji ya kimataifa.
Hata hivyo
bado kuna hatua zingine ambazo zitajadiliwa kataika mkutano mwingine wa Umoja
wa Ulaya unaotazamiwa kufayika leo Alhamisi.
Hayo ya
kijiri, takwimu zinazotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) zinabaini kwamba
watu 800 walikufa maji katika ajali ya boti iliyotokea usiku wa Jumamosi
kuamkia Jumapili Aprili 19, baada ya boti waliyokuwemo kuzama katika bahari ya
Mediterranean. Boti hilo lilikua lilibeba mamia ya wahamiaji. Takwimu hizi
zimetolewa kulingana na ushahidi uliyotolewa na manusura 28 kila waliowasili
Catania, Sicily.
AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KYERWA LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) LEO MKOANI MOROGORO
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete (pichani kati) na Waziri
Mkuu Mh.Mizengo Pinda (pichani shoto) wakishuhudia askari wa jeshi la
Wananchi (JWTZ) wakipiga risasi hewani kama sehemu ya heshima ya kumuaga
aliyekuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera leo,Marehemu Luteni
Kanali Benedict Kitenga (mstaafu) huko kwenye makaburi ya Mlima Kola
Kigurunyembe mkoani Morogoro. PICHA NA IKULU.
Source:fullshangwe blog
Waandamana kupinga ubaguzi Afrika Kusini
Maelfu ya raia wa
Afrika Kusini wanaandamana kupinga wimbi la visa vya hivi majuzi vya
mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni.
Mikutano mikubwa imeandaliwa katika mji
mkuu Johannesburg na katika mji wa Port Elizabeth ulioko kusini mwa nchi hiyo
ambao ulishuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya kigeni
mnamo mwaka 2008.
Makundi ya kiusalama yanafanya misako
katika majumba ya makaazi katika mji wa Alexandra mjini Johannesburg, mahala
ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya raia wa kigeni hasa Afrika yalifanyika
katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, kuonekana
kwa walinda usalama barabarani kumeleta udhibiti na amani.
Source:bbcswahili.com
Saturday, April 4, 2015
Mpango wa Nyuklia wa Iran : makubaliano yafikiwa
Kwa siku ya nane ya mazungumzo kati ya Kundi la nchi 6 zenye nguvu
duniani na Iran katika mji wa Lausanne Alhamisi jioni Aprili 2, makubaliano
kati ya pande mbili hatimaye yamefikiwa.
Iran na serikali za Magharibi wamesema "vigezo
muhimu" kwa "mfumo wa makubaliano" au "hatua" hatimaye
zimepigwa.
"vigezo muhimu" kwa mfumo wa makubaliano kuhusu
mpango wa Nyuklia wa Iran vimepatikana, ametangaza mkuu wa sera za nje wa Umoja
wa Ulaya, Federica Mogherini, katika mkutano na vyombo vya habari, akiwa pamoja
na mwenziye wa Iran katika mji wa Lausanne. Maneno haya yametumiwa na upande wa
Iran pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Umoja wa Ulaya na Marekani watasitisha vikwazo vyote vya
kiuchumi na kifedha vinavyohusiana na nyuklia. " Tuko mbioni sasa
kuandika rasimu ya Nakala ya mpango wa utekelezaji wa pamoja, ikiwa ni pamoja
na maelezo ya kiufundi katika wiki na miezi ijayo", amesema Federica.
|
Ni kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo Rais wa Iran
Hassan Rouhani akifuatiwa na viongozi kadhaa wa nchi za Magharibi wametoa
taarifa kwamba makubaliano kuhusu masuala nyeti ya mpango wa nyuklia wa Iran
yamepatiwa ufumbuzi. Zoezi la kuandika makubaliano ya mwisho linaweza kuanza
mara moja, kwa mujibu wa Hassan Rouhani. Mkataba wa mwisho unaweza kutiliwa
saini " Juni 30", Iran imethibitisha.
Makubaliano haya ya msingi yanaeleza kwamba theluthi mbili
ya uwezo wa sasa wa Iran wakurutubisha uranium usitishwe na kufuatiliwa kwa
kipindi cha miaka kumi, kwa mujibu wa chanzo cha Magharibi. vituo 6000 kwa
jumla ya 19000 vinavyorutubisha uranium vitafuatiliwa, vyombo vya habari vya
Iran vimethibitisha. " Uwezo wa kuipa thamani ya juu uranium
kutoka Iran utapunguzwa", amesema Federica Mogherini.
Burundi : Spika wa bunge azuiliwa kusafiri
Joto la kisiasa limeendelea kupanda nchini Burundi kufuatia
nia ya rais Pierre Nkurunziza ya kugombea muhula wa tatu, huku wafanyakazi wa
serikali wanaopinga kugombea kwa Pierre Nkurunziza muhula wa tatu wakifutwa kazi.
Wakati
huohuo, Spika wa Bunge nchini Burundi, Pie Ntavyohanyuma amezuiliwa Alhamisi
wiki hii kusafiri kwenda nchini ubelgiji katika ziara ya kikazi. Wizara ya
fedha imemuomba kiongozi huyo kutoa maelezo kuhusu matumizi ya Euro elfu
thelathini aliyopewa alipofanya ziara ya kikazi nchini Kenya. Lakini wengi
wanaona kwamba kuzuiliwa kwa Spika huyo, kunaambatana na malumbano yanayojiri
wakati huu katika chama madarakani Cndd-Fdd.
Aliyekuwa
kiongozi wa chama cha Cndd-Fdd, Hussein Radjabu ameikosoa nia ya rais
Nkurunziza ya kutaka kugombea muhula watatu, akisema kwamba iwapo rais huyo
atafanya hivyo atakua amewakosea wafuasi wa chama cha Cndd-Fdd pamoja na raia
wa Burundi kwa ujumla.
Hayo
yakijiri, wito uliyotolewa na mashirika ya kiraia wa kuwataka raia popote pale
walipo kupiga honi, firimbi na kogonganisha vyuma saa sita mchana Alhamisi
Aprili 2, umeitikiwa mjini Bujumbura na katika sehemu mbalimbali za nchi.
Jumatano
wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari kiongozi wa muungano wa
mashirika ya kiraia Forsc, Vital Nshimirimana, amesema wito huo kwa raia ni
kama kadi nyekundu anayopewa mchezaji wa soka aliyefanya madhambi, akibaini
kwamba rais Nkurunziza atakua amepewa kadi nyekundu.
Hayo
yanajiri wakati Kaskazini mwa nchi hiyo, hasa katika mkoa wa Kirundo zaidi ya
raia 300 wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda, wakisema wanahofia usalama wao
kutokana na hali inayojiri wakati huu nchini mwao. Waziri wa Rwanda mwenye
dhamana ya wakimbizi, Serafine Mukantabana amesema serikali yake imejenga kambi
mbili ambapo watapewa hifadhi wakimbizi hao.
Waziri
Mukantabana ameongeza kuwa wako mbioni kuwapatishia matibabu baadhi ya
wakimbizi ambao wameanza kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Kila lakheri Young Africans
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania
kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika Young Africans, katika mchezo wa
marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye
uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.
Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi
walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka
ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia
katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de
Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
Waandamana dhidi ya Al-shabaab Garissa
Wananchi wa mji wa Garissa nchini
Kenya wamefanya maandamano kupinga vitendo vya kundi la Al Shabaab,
lililoshambulia chuo kimoja kikuu mjini humo na kuwaua watu 147 wengi wao
wakiwa wanafunzi hapo jana.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sdUxW8gTRVI23YhvKyVJ7nSTg0mrj3MOZr3QVbHkbSbKeLbmteuLfqSloGJdx42Ams4d7CKka08Ppjqz0USjEzqK99qQy-SjUik9u56O0pTqgQH_qE3auTusMa0jefP3w2Cumr0fJotMT1i9S4uEFcO73AOw5bRFP3dwXqMshnZU84F9-0jP8WpQfML_G_uIloDgEzUSFHDJxlOcNxHfKKNA=s0-d)
Waandamanaji
pia wameelezea kutoridhika na vyombo vya usalama nchini humo wakisema
havikuchukua hatua za kutosha kutoa ulinzi kwa waliouawa na kwa raia wengine
kwa jumla.Wazazi,
jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu cha Garissa wamekuwa
wakiendelea kuwasili katika eneo hilo kuitambua miili ya wapendwa wao.Waliojeruhiwa
wanaendelea kupata matibabu .
Kwa hisani ya BBC Swahili
Subscribe to:
Posts (Atom)