Thursday, July 25, 2013
Rais Kiir avunja baraza la mawaziri
![]() |
| Rais wa Sudan kusini,Salva Kiir |
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir,
amelivunja baraza lake la mawaziri pamoja na kumfuta kazi makamu wa rais Riak
Machar katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya
miaka miwili ya taifa hilo.
Aliyekuwa waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia
BBC kuwa mawaziri wote kutoka kwa Makamu wa Rais Riek Machar wameondolewa.
Duru zinasema haijabainika iwapo kuna waziri yeyote miongoni mwa
wale waliofutwa kazi atarejeshwa katika baraza jipya la mawaziri
litakalobuniwa.
Pia hakuna sababu iliyotolewa kuhusiana na hatua ya rais
kuwafuta kazi maafisa hao , lakini wadadisi wanasema kuwa Bwana Kiir na makamu
wake Machar wamekuwa na mgogoro wa mamlaka kwa miezi kadhaa sasa.
Sudan Kusini imekumbwa na matatizo chungu nzima hasa ya kiuchumi
tangu kujitenga na Sudan mwaka 2011.
Uthabiti wake umetatizwa na malumbano kati yake na Sudan kuhusu
mipaka na swala la mafuta.
Hivi karibuni baadhi ya maafisa wa Bwana Kiir, wamekuwa
wakizungumzia kuwepo minong'ono kuhusu uongozi wake.
Ripoti zinasema kuwa Kiir anajitahidi kusalia na ushawishi
katika chama cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM), ambacho kinathibiti
serikali.
Kwa upande wake bwana Machar, ambaye mwezi Aprili alipunguziwa
mamlaka, alisema huenda akagombea uongozi wa chama cha SPLM dhidi ya rais Kiir,
kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
Kuvunja baraza la mawaziri ni dalili ya juhudi kubwa za rais
kubadilisha sio tu serikali yake bali pia mamlaka na njia za kuingia madarakani
nchini humo.
Ingawa mabadiliko yaliyotangazwa jana yamekuwa yakitarajiwa,
wakati wa kutangazwa kwake ndio umeleta shaka na wasiwasi kuwa rais huenda
anatumia mamlaka yake kubana upinzani na kuzuia mgawanyiko katika serikali
yake.
IGP Mwema, Tendwa wakamia CHADEMA
JESHI la Polisi nchini na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wanaonekana kuanza mkakati maalumu wa kukidhoofisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwaandama viongozi wake kuhusu ushahidi wa mlipuko wa bomu jijini Arusha na mpango wa kutaka kuanzisha kambi ya mafunzo ya ukakamavu kwa vijana kwa ajili ya ulinzi.
Kutokana na mlipuko huo wa bomu Juni 15 mwaka huu, eneo la Soweto jijini Arusha ulioua watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 60 katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, CHADEMA ilitangaza kuanza mpango wa kutoa mafunzo kwa vijana wake kwa ajili ya kulinda mikutano na viongozi wake.
Hata hivyo, msimamo huo wa CHADEMA ulitafsiriwa tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Said Mwema, na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa wakidai hatua hiyo ni kinyume cha sheria za nchi, katiba na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.
Kauli hizo zilipokelewa kwa mtazamo tofauti na wadau wa siasa nchini wakihoji jeshi hilo na Tendwa walikuwa wapi kwa kutoionya CCM yenye kikundi cha vijana cha Green Guard ambacho kinapewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya shughuli za chama.
Licha ya vyombo vya habari kuonyesha picha kadhaa za mafunzo ya kikundi hicho cha CCM kikiwa na vijana wenye silaha, polisi na Tendwa wamekuwa na kigugumizi cha kuzungumzia jambo hilo badala yake wameendelea kuwatisha viongozi wa CHADEMA kuachana na mpango huo.
Katika suala hilo, Tendwa amekuwa na kauli za kujikanganya huku naye akikwepa kuizungumzia Green Guard wakati viongozi waandamizi wa polisi nao wamekuwa na ndimi mbili zinazokinzana kwenye suala hilo ambalo wamelibebea bango wakitaka kufifisha tukio la mlipuko wa Arusha.
Jumamosi iliyopita, gazeti hili lilichapisha barua iliyoandikwa na ofisi ya Tendwa kwenda kwa CHADEMA yenye kumb. Na RPP/CHADEMA/72/32 ikikiruhusu chama hicho kuanzisha vikundi vya ulinzi na usalama kama ilivyo katika katiba yao.
Ofisi hiyo ya msajili kupitia kwa Naibu Msajili, Sisty Nyahoza, jana ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikikana kuwahi kutoa ruhusa kwa CHADEMA au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote.
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha kuwa Tendwa anaibeba CCM, licha ya kutoa vitisho kwa CHADEMA kuwa atawachukulia hatua za kisheria endapo watashindwa au kukataa kutii agizo la kutoanzisha makambi hayo, hakusema chochote kwa chama tawala ambacho kinaendesha kambi za kujihami.
Julai 9 mwaka huu, CHADEMA kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, walisema kufuatia mlipuko wa bomu Arusha, chama hicho kinakusudia kuanzisha kambi za mafunzo kwa vijana watakotumika kulinda viongozi katika shughuli zake kutokana na Jeshi la Polisi kushindwa kuchukua hatua stahiki.
Siku chache baadaye, Mbowe alivamiwa usiku wa manane nyumbani kwake na askari kadhaa wakidai kuwa walitaka awapatie ushahidi wa video ya mauaji aliyodai kuwa nayo ikiwaonyesha baadhi ya polisi walivyoshiriki kwenye tukio la mlipuko wa bomu Arusha.
Baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa kufichua tukio hilo kwenye mkutano wa hadhara kesho yake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alidai hana taarifa za askari wake kufika nyumbani kwa Mbowe kumkamata.
Jeshi hilo kisha liligeuza hoja na kumtaka Mbowe ajisalimishe kwa ajili ya mahojiano kuhusu kauli yake ya kuhusu chama kutaka kuanzisha makundi ya mafunzo ya ukamamavu kwa vijana wao.
Julai 17 mwaka huu, Mbowe aliandikiwa barua akiamrishwa awasilishe ushahidi wa video aliyodai kuwa nayo, ikiwaonyesha baadhi ya polisi walivyoshiriki kwenye tukio la mlipuko wa bomu Arusha.
Wakati Mbowe akiamriwa kufanya hivyo kabla ya juzi saa nane mchana, jeshi hilo halijawahi kuwahoji Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ambao walinukuliwa wakidai wana ushahidi kwamba CHADEMA walijilipua wenyewe.
Juni 20 mwaka huu, Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa jeshi hilo, Paul Chagonja aliwaeleza wanahabari kuwa Mbowe anapaswa kuwa mkweli na kuacha kuuchezea umma kwani alichowaeleza polisi ni tofauti akisema hana ushahidi huo wa mlipuko wa bomu bali alielezwa na wafuasi wake.
Lakini katika hatua ya kushangaza, Chagonja huyo huyo ndiye amemwamuru Mbowe tena kupeleka ushahidi huo polisi akitamba kuwa baada ya kukaidi kufanya hivyo, polisi inao makachero wake wanaojua jinsi gani ya kuendelea na kazi hiyo.
Muda aliopewa Mbowe umemalizika bila kuwasilisha ushahidi huo, akidai kuwa hawezi kwenda kinyume na msimamo wa chama kwani walikwishamwandikia Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka aunde tume huru ya majaji ndipo watapeleka ushahidi wao huo na mwingine.
Mbowe alisema kuwa jeshi hilo ni watuhumiwa, hivyo kamwe hawawezi kupeleka ushahidi huo kwao, na kukitaka chombo hicho cha dola kufungua kesi mahakamani ili CHADEMA wapeleke ushahidi huo huko.
Jana, Mbowe alijisalimisha tena polisi kama alivyokuwa ameamriwa, lakini hakupeleka ushahidi huo, na jeshi hilo lilimwamuru tena kupeleka ushahidi huo kwa maandishi Ijumaa wiki hii.
source:Tanzania Daima

Wednesday, July 24, 2013
TAHADHARI
Kuna taarifa ya utapeli hatari umeingia mjini..watu wanajifanya wanauza manukato(perfumes).Watakushawi shi unuse kipande cha karatasi ambacho kimenyunyuziwa dawa yenye sumu ambayo ukinusa tu unaweza kujikuta umepoteza fahamu na hapo unawapa nafasi ya kuibiwa ulicho nacho.Tafadhari kuwa mwangalifu unapokutana na watu kama hao.
Mtumie ujumbe huu pia ndugu na rafiki yako na watu wote unaowajali .
Mtumie ujumbe huu pia ndugu na rafiki yako na watu wote unaowajali .
Rais Kikwete atoa maelekezo kuhusu kodi ya simu za mkononi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.
Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.
Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.
Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
23 Julai, 2013
Tuesday, July 23, 2013
Sherehe London kwa kuzaliwa mwanamfalme
| Tangazo la kuzaliwa mwana Mfalme likitolewa |
Ujumbe wa heri njema umeendelea
kutolewa kutoka kote duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa
tatu kwenye foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.
Mwanamfalme William na mkewe Kate
,wameamkia hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa
kwanzaJumatatu jioni.
Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na
takriban kilo tatu na nusu atafahamika kama mwanamfalme wa Cambridge, lakini
hajapewa jina.
Katika taarifa fupi William,amesema
wana furaha isiyo na kifani.
Baadaye leo jeshi la Uingereza
linatarajiwa kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40
hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.
Kawaida saluti ambayo hutolewa kwa
mwanamfalme huwa ni mizinga ishirini na moja lakini huongezeka hadi arobaini na
moja ikiwa itarushwa kutoka katika makao ya kifalme
Taarifa kutoka katika Kasri la
Buckingham, zinasema kuwa Malkia Elizabeth na mumewe walifurahishwa sana na
habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo. Naye babake William
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Waziri mkuu wa Uingereza David
Cameron, alisifu sana kuzaliwa kwa mtoto huyo na kuitaja kuwa hatua muhimu sana
kwa Uingereza.
Naye waziri mkuu wa Australia, Kevin
Rudd, alitaja sherehe za jana kama muhimu sana kwa nchi za juimuiya ya madola,
huku akiongeza kuwa watu wa Australia wanampenda sana Prince William baada ya
kuzuru nchi hiyo akiwa mtoto mwenyewe.
Urine-Powered Fuel Cell Charges Mobile Phone
What do you think of the Bristol scientists’ experiment? Would you use a urine-powered fuel cell to charge your devices?
Thursday, July 18, 2013
Kodi ya kadi ya simu (SimcardTax): Maoni ya awali ya wananchi juu ya hatua za kuchukuliwa
Nawashukuru kwa maoni ambayo mmenitumia kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa kufuatia kuanzishwa kwa ushuru wa bidhaa kwa kadi za simu (sim card) kwa wamiliki wa simu za kiganjani/mkononi.
Bado naendelea kuchambua maelfu ya maoni yaliyotolewa katika mijadala na niliyotumiwa kwa barua pepe. Nitoe mrejesho wa awali kwamba kwa muktasari mapendekezo niliyoyachambua mpaka sasa yanapendekeza hatua zifuatazo kuchukuliwa:
Kwanza, taarifa itolewe kwa wanahabari na umma yaliyojiri na yatokanayo na kupitishwa kwa kodi hiyo;
Pili, hatua zisiwe kwa kodi hii pekee yake bali zote zenye kuongeza gharama za maisha kwa wananchi.
Tatu; majina ya wabunge wanaodaiwa kutoa mawazo ya kupendekeza kodi hiyo kutozwa yatajwe;
Nne, muswada wa sheria upelekwe bungeni katika mkutano ujao kufuta kodi hiyo;
Tano, saini za wananchi zikusanywe kupinga kodi hiyo na kuwasilishwa bungeni au kwa Serikali;
Sita, Serikali itakiwe kusitisha utekelezaji wa kifungu husika cha sheria hiyo ili wananchi wasianze kubebeshwa mzigo huo wa gharama;
Saba, maandamano yaandaliwe kulaani kupitishwa kwa kodi hiyo na kutaka utozaji wa kodi hiyo usianze kutekelezwa;
Hatua ambazo tayari zimeanza kuchukuliwa:
Wakati nikiendelea na uchambuzi nimeanza pia kuchukua hatua namba moja mpaka tano. Nashukuru pia kwa upande wenu baadhi mmeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kukusanya saini kupitia link hii:http://www.avaaz.org/en/
Aidha, natoa mwito kwa kila mwananchi aliyeguswa na suala hili kwa kutumia haki yake kwa kuzingatia wajibu muhimu kuwezesha hatua mbalimbali kuchukuliwa kwa kurejea mapendekezo yaliyotolewa.
Kwa upande wangu; Mosi, kupitia mkutano wa hadhara tarehe 13 Julai 2013 na njia nyingine niliendelea na mchakato ulionza kabla ya mkutano wa kumi na moja wa Bunge kuanza wa kukusanya saini za watu wanaotoa madai ya kutaka Bunge liisimamie Serikali kupunguza athari za ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi na kudhibiti mfumuko wa bei nchini. Mpaka sasa zimeshafika saini 23569.
Yeyote anayetaka kukusanya saini za wengine katika eneo lake naomba awasiliane na Afisa katika ofisi ya mbunge Gaston Garubimbi (0715/0767-825025) kwa ajili ya kutumiwa fomu.
Aidha, nitashiriki mkutano wa hadhara jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni. Hivyo, kwa wale mlio katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam mnaalikwa kuhudhuria mkutano huo ambapo mtapata pia fursa ya kusaini fomu tajwa.
Mkutano huo unalengo la kutoa mrejesho kuhusu yaliyojiri bungeni katika mkutano uliopita na kupokea masuala ya kuyawasilisha katika mkutano ujao. Aidha, uchambuzi utafanyika kuhusu rasimu ya katiba sanjari na juu ya mchakato wa katiba mpya.
Pili, tarehe 15 Julai 2013 niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuwasilisha muswada binafsi wa sheria kuwezesha kufutwa kwa ushuru tajwa. Katika barua hiyo nimeomba masharti ya kanuni ya Kanuni ya 21(1) (d) (e) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge yazingatiwe kuniwezesha kuchukua hatua hiyo katika Mkutano wa kumi na mbili wa Bunge uliopangwa kuanza mwezi Agosti 2013. Hivyo, yeyote ambaye angependa kujitolea 3M (Maarifa, Muda au Mali) kufanikisha maandalizi ya muswada huo awasiliane nasi kupitia barua pepe mbungeubungo@gmail.com. Maslahi ya umma Kwanza.
John Mnyika (Mb)
18 Julai 2013
Tuesday, July 16, 2013
Darfur tragedy: How they were attacked
The slain soldiers, who were part of the UN-Africa Mission in Darfur (Unamid) died on Saturday after gunmen ambushed a convoy comprising Tanzanian peacekeepers. Their 17 colleagues were seriously wounded in the incident described as the deadliest ever single attack on the international force in Sudan.
The unidentified assailants ambushed the convoy of the African Union and the United Nations Hybrid Operation in Darfur at Khor Abeche in southern Darfur, killing the seven Tanzanian soldiers instantly.
TPDF spokesman, Colonel Kapambala Mgawe, said on Sunday that a team of experts would travel to Khartoum and Darfur for talks with authorities over the attack.
Speaking from Sudan, a police officer who working in Nyala town, Darfur and who preferred anonymity for fear of reprimand toldThe Citizen yesterday that the attack occurred when the soldiers were on a search for UN vehicles which are said to have been stolen by a rebel group.
“The soldiers were in a normal patrol, but a week ago, unknown assailants attacked members of the army and disappeared with four vehicles without causing any injury,’’ he said, adding:
“On Saturday our soldiers saw their vehicles parked somewhere, but when they moved to recover them, they were suddenly and viciously attacked.”
He described the incident as the biggest and that the surviving soldiers are engulfed in fear. “It is really traumatising here; I can tell you the rebels are fully armed with sophisticated weapons’’, said the police.
He added that of all the incidents he has witnessed while working as a security man, the one on Saturday was the most vicious.
As of yesterday, the TPDF was yet to reveal the names the fallen Tanzanians. Colonel Mgawe said the army was communicating with the UN in part of the process to bring the soldiers’ remains home. He, however, declined to give names.
“It is too early to divulge the names, but we are all set to receive their bodies which will be transported here by the UN,” he said.
Yesterday, Unamid spokesperson Chris Cycmanick, told The Citizen that plans to bring the bodies to Tanzania were underway and that by the end of the week, they would be in Dar es Salaam.
SourceThe Citizen
Majambazi yateka mabasi mawili
Kagera. Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameteka mabasi mawili ya abiria na kufanya uporaji katika Pori la Hifadhi ya Biharamulo Mkoani Kagera na kupora bunduki aina ya SMG iliyokuwa na askaRi aliyekuwa anasindikiza mabasi hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Alisema silaha zilizoonekana eneo la tukio ambazo zilitumiwa na majambazi kujihami ni SMG sita na LMG mbili.
Kwa mujibu wa Kalangi, mabasi yaliyotekwa ni NBS lililokuwa likielekea Arusha na RS lililokuwa likielekea Dar es Salaam,ambapo kabla waliteka gari dogo na kulitumia kufunga barabara katika hali iliyoonekana lilikuwa limeharibika.
Katika tukio hilo, abiria mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Fredrick Rugaihura (47)mkazi wa mjini Bukoba alijeruhiwa shingoni kwa risasi, ambapo majambazi hao walipora mali mbalimbali za abiria zikiwemo fedha na simu.
Source:Mwananchi
Monday, July 15, 2013
MAJINA YA ASKARI WA TANZANIA WALIOUWAWA DARFUR HAY HAPA
Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa muda mfupi uliopita kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.
Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.
Wakati wakiwa wakijiandaa, ghafla wakazingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina

Thursday, July 11, 2013
Safari ya kupata elimu
Sylivia ni msichana wa miaka 8 anayeishi katika kijiji kimoja nchini Tanzania.Ni msichana anyetoka kijijini akipigania elimu yake.
Fuatilia safari yake ya kupata elimu katika picha
Fuatilia safari yake ya kupata elimu katika picha
![]() |
| Sylivia akiagana na mama yake tayari kuanza safari yake kwenda shuleni |
![]() |
| Hii ni sehemu ya njia ambayo anapitia Sylivia kwenda na kurudi shuleni,Je ni salama kwake? |
![]() |
| Sylivia akielekea shuleni |
![]() |
| Sylivia kiingia eneo la shule |
Marekani kutoa ndege za kivita Misri
Marekani inaendelea
na mpango wake wa kutoa ndege za kivita kwa jeshi la Misri licha ya msukosuko
wa kisiasa unaokumba nchi hiyo. Hatua hii inajiri wakati Marekani ikiendelea
kutathmini matukio ya wiki jana ambapo jeshi lilimuondoa madarakani Rais
Mohammed Morsi.
Msaada wa kijeshi kwa
Misri ungesitishwa endapo Marekani ingelitaja matukio ya wiki jana kama
mapinduzi ya kijeshi. Kundi la Muslim Brotherhood linalomuunga mkono Morsi
linasisitiza arejeshwe madarakani
Wafuasi wake wamekua wakiandamana karibu na
kambi kuu ya jeshi ambapo anaaminika kuuzuiliwa. Hapo Jumatatu,wafuasi wa
Brotherhood 51 waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi wakati wanakabiliano.
Utawala wa mpito umesema kwamba Bw. Morsi
anazuiliwa eneo salama na kwamba haki zake zinazingatiwa.Maafisa wa Marekani
wamesema ndege mpya za kivita aina ya F-16 zitawasilishwa katika wiki chache
zijazo.
Mpango wa kufadhili jeshi ulianza kutekelezwa
mapema mwaka huu na jeshi inatarajia kupokea ndege 20 za kivita. Msemaji wa
ikulu ya Rais amesema Marekani haitabadilisha mpango wa kufadhili jeshi la
Misri, japo inaendelea kutathmini kuhusu matukio ya kisiasa. Msaada wa kijeshi
nchini Misri ambao hutolewa na Marekani hufikia dola bilioni 1.3 kila mwaka.
Hapo Jumanne, kibali cha kumkamata kiongozi wa
Muslim Brotherhood Mohamed Badie kilitolewa pamoja na wakuu wengine tisa wa
kundi hilo. Viongiozi hao wamelaumiwa kwa kuchochea ghasia mjini Cairo ambapo
zaidi ya watu 50 waliuawa na mamia kujeruhiwa.
Tuesday, July 2, 2013
USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA : Simba yanasa vifaa vitatu
Dar es Salaam. Katika kuhakikisha haifanyi makosa zaidi, klabu ya Simba juzi iliwasainisha wachezaji watatu, Sino Agustino, Marcel Kaheza ‘Rivaldo’ na Omary Salum ‘Inzagi’.
Sino ni mshambuliaji amesajiliwa na Simba akitokea Prisons ya Mbeya kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo mshambuliaji Malceli na beki wa kushoto Omary wamepandishwa kutoka Simba B.
Wachezaji hao wakisaini kwenye ofisi za Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia usajili huo, Itang’are alisema,”Katika kuhakikisha hatufanyi makosa tumemalizana na wachezaji hawa kwa lengo la kuiboresha timu katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.”
Alisema,”Tumewasajili vijana hawa baada ya kufanya majaribio na makocha wameridhika na viwango vyao kwa kipindi chote cha majaribio,”alisema Itang’are.
Naye, Sino akizungumzia kusajiliwa na Simba alisema amefurahishwa na benchi la ufundi la Simba kwa kumwamini na kumjumuisha kikosini hapo, hivyo ameahidi kuifanyia kazi nzuri klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi.
“Nashukuru kuchaguliwa Simba, nawaahidi mashabiki nitawafanyia kazi nzuri, kikubwa naomba ushirikiano wao,”alisema Sino.
Naye Malcel alisema,” Nimefurahi kusajiliwa Simba na sasa najipanga kuhakikisha naifanyia mazuri klabu hii kwenye ligi na mashindano mengine yatakayotukabiri.”
Kwa upande wa Omary yeye alisema atajitoa kwa nguvu zote kuifanya Simba ing’are.
Tayari Simba imempa mkataba tena Amri Kiemba, imemsajili beki Samwel Senkoon raia wa Uganda kutoka URA, imemsajili Andrew Ntala kutoka Kagera Sugar, Ibrahim Twaha ‘Messi’ kutoka Coastal Union ya Tanga na wengine wa timu B kama Ramadhani Singano ‘Messi’, Hassan Khatib na Edward Christopher.
Katika hatua nyingine, Simba iliifunga timu ya Kiluvya bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Bao hilo la Simba lilifungwa na Sino kutokana na pasi ya Malcel.
Source:Mwananchi
Obama, Bush ana kwa ana Tanzania
Rais wa Marekani, Barack Obama na mtangulizi wake, George W. Bush, leo wanakutana ana kwa ana kwenye ardhi ya Tanzania watakapoweka mashada kwenye Ubalozi wa zamani wa Marekani uliolipuliwa mwaka 1998.
Rais Obama ameweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuongoza Marekani, akipokea wadhifa huo kutoka kwa Rais Bush, ambaye aliiongoza taifa hilo kuanzia mwaka 2000-2008.
Kitendo cha vigogo hao kukutana nchini ni cha
kihistoria na kinadhihirisha jinsi Marekani ilivyoipa kipaumbele Tanzania kwa masuala ya diplomasia.
Viongozi hao wawili, wapo Tanzania wakati Rais Obama akimalizia ziara yake ya Afrika na Bush atakuwa na mkewe, Laura, watahudhuria mkutano wa wake za marais wa Afrika unaodhaminiwa na Taasisi ya Bush Foundation.
Pia, Michelle Obama, atahudhuria mkutano huo kabla ya kuondoka kurejea Marekani.
Balozi mbili za Marekani za Dar es Salaam na Nairobi, Kenya zilishambuliwa kwa wakati mmoja Agosti 7, 1998.
Obama ataweka shada kama sehemu ya kumbukumbu ya tukio hilo na Bush ataungana naye katika shughuli hiyo.
Hata hivyo, viongozi hao hawatahutubia wakati wa shughuli hiyo.
Rais Obama ametoa pongezi kwa sera za Bush Afrika hasa kwa kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Hata hivyo, utawala wa Rais Obama umejikita zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Kuna kamandi ya Jeshi ya Africom, ambayo ina kazi kubwa ya kukabiliana na ugaidi barani humu.
Source:Mwananchi
Monday, July 1, 2013
Pesa za misaada zinavyofujwa Afrika
Kamati ya Bunge la Uingereza limepokea taarifa kuwa zaidi ya dola milioni
650 pesa za msaada zilizotolewa na mataifa ya Ulaya kwa bara la Afrika
zimetumiwa vibaya.
Kamati ya bunge la
malodi kuhusu maswala ya nje, inachunguza ambavyo dola bilioni 1.3 zilizotolewa
kama msaada kwa miradi ya maji kusini mwa jangwa la Sahara miaka kumi
iliyopita, zilivyotumiwa.
Kamati hiyo iliarifiwa
kuwa chini ya nusu ya miradi 23 iliyochunguzwa ilikuwa duni na wala haikutimiza
mahitaji ya wananchi.
Matatizo yalitokana na
mipango duni na hata wakati wa kuitekeleza miradi mipango haikuwa sawa.
Mkaguzi mmoja wa
matumizi ya pesa aliambia kamati hiyo kuwa utafiti wake ulionyesha wazi hali ya
miradi mingine ambayo ilifanywa na Muungano wa Ulaya katika mwongo mmoja
uliopita.
Miradi ya maji
hujumuisha utoaji wa huduma za maji safi, ujenzi wa vyoo hatua ambazo zinazuia
kulipuka kwa magonjwa.
Wakaguzi pia
waligundua kuwa vifaa vilivyonunuliwa na mameneja wa miradi kama paipu vilikuwa
vinahitajika.
Matatizo yanatokana na
ikiwa miradi hiyo inaweza kudumu au la.
Katika visa vingine,
idadi ya wenyeji wanaopokea mafunzo ni ndogo sana kwa hivyo baada ya miradi
kutekelezwa haiwezi kudumu.
Lakini tatizo kubwa
zaidi lilikuwa ufadhili au kuwepo mikataba ya kudumu kutoka kwa kamati na
serikali za nchi maskini kuhusu namna ya kufadhili mfano hiyo miradi ya maji.
Ikiwa mikataba haiwezi
kuwekwa basi itakuwa vigumu kwa matumizi mazuri ya pesa na pia kuna hatari ya
pesa za maendeo kuendelea kufujwa.
Makao ya chama kikuu yavamiwa Misri
![]() |
| Sehemu ya waandamaji |
Waandamanaji
wanaopinga serikali nchini Misri, wamevamia makao makuu ya chama tawala cha
Muslim Brotherhood mjini Cairo.
Inaarifiwa wamepora
mali iliyokuwa kwenye ofisi hizo katika mji wa Moqattam wakitupa baadhi ya vitu
nje ya madirisha kabla ya kuiteketeza ofisi yenyewe.
Awali, vuguvugu la upinzani lililoandaa maandamano hayo, ambayo yameshuhudia mamilioni ya watu wakijitokeza kuandamana nchini Misri, wametoa makataa kwa rais Morsi hadi Jumanne ajiuzulu.Rais Mohammed Morsi ni rais wa chama hicho cha kiisilamu chenye ushawishi mkubwa.
Taarifa iliyotolewa na kundi hilo, Tamarud au (waasi) ilisema kuwa bwana Morsi huenda akakumbana na raia wasiotii sheria kama njia ya kumuonyesha kuwa wanampinga ikiwa hataondoka mamlakani na kuruhusu uchaguzi kufanyika.
Mamilioni ya watu walihudhuria maandamano, nchini kote Jumapili kumtaka Morsi kuondoka mamlakani.
Pande zote husika zilishangazwa na maandamano yanayofanywa dhidi ya Morsi.
Upinzani ni muungano wa vyama vingi, vikiwemo vianvyomuunga mkono rais aliyeng'olewa mamlakani Mubarak pamoja na watu waliojitolea maisha yao kumuondoa mamlakani.
Changamaoto kwano ni kutafuta njia ya kuendwel;eza maandamno yenyewe hadi wanachokitaka kitakapotimia.
Masemaji wa rais Morsi ameitisha mkutano kati ya pande husika.
Kwa hilo kufanikiwa, rais atahitajika kujitolea na kukubali matakwa yao, ikiwemo hata kufanyia katiba marekebisho.
Hakuonyesha dalili za kutaka mwafaka na wanaompinga, alipokuwa anatoa hotuiba yake wiki jana.
Kwa waandamanaji, wanataka aondoke mamlakani kwa kuitisha uchaguzi wa mapema. Kwa sasa vurugu inaonekana zitaendelea kwa muda.
NI KWELI BARABARA ZA BONGO ZILIPIGWA DEKI KWA AJILI YA UJIO WA OBAMA
Hakikisha mwenyewe kama ni kweli barabara za jijini Dar es salaam zilipigwa deki kwa ajili ya ujio wa Raisi wa Marekani Mh.Barack Obama baada ya kumaliza ziara yake Afrika ya Kusini
Subscribe to:
Posts (Atom)