Kamati ya Bunge la Uingereza limepokea taarifa kuwa zaidi ya dola milioni
650 pesa za msaada zilizotolewa na mataifa ya Ulaya kwa bara la Afrika
zimetumiwa vibaya.
Kamati ya bunge la
malodi kuhusu maswala ya nje, inachunguza ambavyo dola bilioni 1.3 zilizotolewa
kama msaada kwa miradi ya maji kusini mwa jangwa la Sahara miaka kumi
iliyopita, zilivyotumiwa.
Kamati hiyo iliarifiwa
kuwa chini ya nusu ya miradi 23 iliyochunguzwa ilikuwa duni na wala haikutimiza
mahitaji ya wananchi.
Matatizo yalitokana na
mipango duni na hata wakati wa kuitekeleza miradi mipango haikuwa sawa.
Mkaguzi mmoja wa
matumizi ya pesa aliambia kamati hiyo kuwa utafiti wake ulionyesha wazi hali ya
miradi mingine ambayo ilifanywa na Muungano wa Ulaya katika mwongo mmoja
uliopita.
Miradi ya maji
hujumuisha utoaji wa huduma za maji safi, ujenzi wa vyoo hatua ambazo zinazuia
kulipuka kwa magonjwa.
Wakaguzi pia
waligundua kuwa vifaa vilivyonunuliwa na mameneja wa miradi kama paipu vilikuwa
vinahitajika.
Matatizo yanatokana na
ikiwa miradi hiyo inaweza kudumu au la.
Katika visa vingine,
idadi ya wenyeji wanaopokea mafunzo ni ndogo sana kwa hivyo baada ya miradi
kutekelezwa haiwezi kudumu.
Lakini tatizo kubwa
zaidi lilikuwa ufadhili au kuwepo mikataba ya kudumu kutoka kwa kamati na
serikali za nchi maskini kuhusu namna ya kufadhili mfano hiyo miradi ya maji.
Ikiwa mikataba haiwezi
kuwekwa basi itakuwa vigumu kwa matumizi mazuri ya pesa na pia kuna hatari ya
pesa za maendeo kuendelea kufujwa.
No comments:
Post a Comment