Rais Mohamed Mursi aungwa mkono na
Wamisri katika duru ya kwanza ya kura ya maoni juu ya katiba mpya ambayo
anataraji itaitoa nchi hiyo kwenye mzozo wakati wapinzani wakiipinga kwa
kukandamiza haki za jamii ya wachache.
Katika siku ya kwanza ya kura
ya maoni juu ya rasimu ya sheria za msingi za nchi hiyo asilimia 56.5 ya kura
zimeikubali kwa kura ya ndio. Duru ya pili ya kura hiyo ya maoni hapo Jumamosi
ijayo yumkini ikapiga kura nyingine ya ndio kutokana na maeneo mengi
yanayotarajiwa kupiga kura hiyo yana wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu na
hiyo ina maana kwamba katiba hiyo itapita.Lakini wakati kura ya hapana ikiwa ni
asilimia 43 jambo ambalo linaloonyesha kukaribiana kwa matokeo hayo hakumpi
faraja kubwa Mursi kutokana na mgawanyiko mkubwa katika nchi ambapo anahitaji
kuwa na muafaka kwa ajili ya kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi.
No comments:
Post a Comment