Saturday, April 4, 2015

Mpango wa Nyuklia wa Iran : makubaliano yafikiwa

Kwa siku ya nane ya mazungumzo kati ya Kundi la nchi 6 zenye nguvu duniani na Iran katika mji wa Lausanne Alhamisi jioni Aprili 2, makubaliano kati ya pande mbili hatimaye yamefikiwa.
Aprili 2 mwaka 2015, katika mji wa Lausanne, Uswisi, makubaliano ya kisiasa yakifikiwa kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu suala la mpango wa nyuklia wa Iran.
Iran na serikali za Magharibi wamesema "vigezo muhimu" kwa "mfumo wa makubaliano" au "hatua" hatimaye zimepigwa.
"vigezo muhimu" kwa mfumo wa makubaliano kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran vimepatikana, ametangaza mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, katika mkutano na vyombo vya habari, akiwa pamoja na mwenziye wa Iran katika mji wa Lausanne. Maneno haya yametumiwa na upande wa Iran pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Umoja wa Ulaya na Marekani watasitisha vikwazo vyote vya kiuchumi na kifedha vinavyohusiana na nyuklia. " Tuko mbioni sasa kuandika rasimu ya Nakala ya mpango wa utekelezaji wa pamoja, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kiufundi katika wiki na miezi ijayo", amesema Federica.
Ni kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo Rais wa Iran Hassan Rouhani akifuatiwa na viongozi kadhaa wa nchi za Magharibi wametoa taarifa kwamba makubaliano kuhusu masuala nyeti ya mpango wa nyuklia wa Iran yamepatiwa ufumbuzi. Zoezi la kuandika makubaliano ya mwisho linaweza kuanza mara moja, kwa mujibu wa Hassan Rouhani. Mkataba wa mwisho unaweza kutiliwa saini " Juni 30", Iran imethibitisha.
Makubaliano haya ya msingi yanaeleza kwamba theluthi mbili ya uwezo wa sasa wa Iran wakurutubisha uranium usitishwe na kufuatiliwa kwa kipindi cha miaka kumi, kwa mujibu wa chanzo cha Magharibi. vituo 6000 kwa jumla ya 19000 vinavyorutubisha uranium vitafuatiliwa, vyombo vya habari vya Iran vimethibitisha. " Uwezo wa kuipa thamani ya juu uranium kutoka Iran utapunguzwa", amesema Federica Mogherini.


No comments:

Post a Comment