Friday, November 30, 2012

SYRIA BILA MAWASILIANO

Huduma za mtandao na simu zilikatika katika mji mkuu wa Damscus pamoja na maeneo ya katikati mwa Syria.
Kumekuwa na mapigano zaidi huko Damascus na karibu na uwanja wa ndege, kati ya vikosi vya serikali na waasi.
Kulikuwa na safari moja tu ya ndege iliyofanikiwa Alhamisi.
Serikali inasema hali hiyo ilisababishwa na waasi, lakini habari zinaeleza kuwa ni serikali ndiyo iliyokatiza mfumo wa mawasiliano ili kuzuia mawasilaino kati ya wapiganaji waasi.

No comments:

Post a Comment