Monday, April 14, 2014

DARAJA LA MTO MZINGA NA KONGOWE KIGAMBONI LAHARIBIKA VIBAYA

Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha siku ya jumamosi na jumapili zimeleta athari kubwa kwa wakazi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam,ambapo miundombinu na makaazi ya watu yameathiriwa vibaya na mvua hizo na kuacha baadhi ya familia kupoteza ndugu zao na kukatisha usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine.
Hili nililishuhudia jana eneo la Mbagala(Darajani mzinga)ambapo jana asubuhi daraja hili lilikuwa linapitika kwa waenda kwa miguu peke yake na kuacha magari na bodaboda kubaki upande uliokuwepo .Pichani ni baadhi ya sehemu hizo korofi.

Wakazi wa Kongowe wakiangalia maafa yaliyoletwa na Mvua hizo

Roli Kubwa la Mafuta lililotumbikia likijaribu kuvuka kwenye Daraja hilo la Kongowe likitokea Kigamboni

Sehemu ia daraja iliyoondolewa na maji


Wananchi wakijaribu kuvuka kwenda upande wa pili wa daraja baada ya maji ya mto kupungua


Add caption


Kibao kikionyesha kuwa barabara hiyo imefungwa kwa muda


Hapa ni Darajani Mzinga sehemu yalipokuwa yakihifadhiwa mabomba ya gesi

Wachina waliokuwa wakiishi eneo hilo wakiokoa vitu vyao


Jinsi kulivyokuwa kukionekana


Mto Mzinga Umefurika


Umati wa watu wakijaribu kuvuka 

Umati wa watu wakijaribu kuvuka


Daraja limefungwa na wananchi wanapita kwa zamu upande mmoja




Friday, April 11, 2014

Ukraine yawatuliza wanaotaka kujitenga

Waziri Mkuu wa Mpito wa Ukraine
Waziri Mkuu wa mpito wa Ukraine Arsenity Yatsenyuk amewaambia viongozi wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo kwamba amekusudia kuwaongezea madaraka zaidi kwenye eneo hilo.
Hata hivyo hajafafanua ni kwa kiasi gani atawapa mamlaka hayo na kwamba madaraka hayo kama yanaweza kuwaridhisha wakazi wa eneo hilo lenye viwanda la Mashariki mwa Ukraine ambalo linataka kujitenga.
Bwana Yatsenyuk ameutembelea mji wa Donetsk katika jitihada zake za kushughulikia msimamo wa waandamanaji wanaounga mkono Urusi ambao wameteka majengo ya serikali za mtaa na kutangaza uhuru kutoka nchi ya Ukraine.
Wanaharakati pia wameendelea kushikilia majengo ya serikali katika mji wa Luhansk.
Tayari Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuchochea uvunjifu wa amani nchini Ukraine.


UN yatowa onyo kali kwa serikali ya Burundi

Umoja wa Mataifa umetuma onyo kali kwa Serikali ya Burundi na kuitaka kuchukua hatua za haraka kushughulikia vurugu za kisiasa na kuheshimu haki za binadamu. “Tuna imani kwamba serikali ya Burundi itazingatia haraka iwezekanavyo na kushughulikia (matatizo yote) yanayosababisha vurugu na ukiukwaji wa haki za bin adamu”, amesema msemaji wa Umoja wa Matiafa Stéphane Dujarric.
Aidha, umoja huo umebainisha kuwa endapo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na uchochezi wa vurugu vitaendelea, basi wahusika watawajibika mbele ya mahakama za kimataifa.
“iwapo hakutochukuliwa hatua, huku ukiukwaji wa haki za binadamu zikiendelea, hatutosita kuwachukuklia hatua za kisheria wahusika, na ikiwezekana wafikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa wajibu tuhuma zinazowakabili”, ameendelea kusema Dujarric.
Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kitengo cha kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng yuko ziarani mjini Bujumbura, ambako atajadili hofu hio ya kutokea kwa mauaji ya kimbari na viongozi wa Burundi.
Onyo hilo ni miongoni mwa tahadhari ziliyokua zikitolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa pamoja na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power.
Akiwa ziarani mjini Bujumbura hivi karibuni, balozi Samantha Power, aliwatajka viogozi wa Burundi kuheshimu uhuru wa kisiasa, na vilevile kuheshimu katiba ya nch, ambayo utawala unajaribu kuifanyiya marekebisho.
 Tunasisitiza kuheshimu katiba ya nchi, ambayo ni sheria mama ya Burundi, na vilevile kuheshimu haki za binadamu,” alisema Samantha Power baada ya mazungumzo na rais Pierre Nkurunziza.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilielezea aprili mosi wasiwasi wake, juu ya mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.
Katika tangazo liliyotolewa jana alhamisi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeelezea kwa mara nyingine wasiwasi wake juu ya uhuru wa kujieleza na mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa vya upinzani na mashirika ya kiraia.
Wajumbe 15 wa baraza hilo, wameelezea wasiwasi wao juu “ya vitisho na kufungwa kiholela pamoja na machafuko yanayotekelezwa na vijana kutoka vyama vya kisiasa”.
Wajumbe hao wametoa wito kwa serikali ya Burundi kutowafumbia macho wafuasi wa chama tawala ambao wamekua wakijihusisha na maovu mbalimbali, mkiwemo unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa wiki kadhaa Umoja wa Mataifa umepata taarifa za kuaminika za usambazaji wa silaha na sare za kijeshi kwa vijana wa chama tawala Imbonerakure, shutuma ambazo zimetupiliwa mbali na serikali ya Burundi.
Ni kweli kwamba kumekuwepo na matukio ya vurugu baina ya vijana wa vyama mbalimbali vya kisiasa na sio tu chama tawala. Pia hakuna hali ya kutokuwajibika kwa sababu uchunguzi unafanyika kuhusiana na matukio hayo na tunapenda kuwaambia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa nchi ya Burundi haisanbazi silaha kwa vijana wa chama hicho tawala”, naibu msemaji wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe.
Burundi inapitia wakati huu mgogoro mkubwa wa kisiasa kutokana na mgawanyiko kati ya chama cha rais Pirrea Nkurunzia, chenye wahutu wengi na chama cha UPRONA, chenye watutsi wengi.
Bunge la Burundi lilikataa katikati ya mwezi wa machi kuidhinisha mswada wa sheria ya kufanya marekebiho ya katiba, ambayo kwa mujibu wa upinzani ingelisababisha taifa hilo kuingia katika dimbwi la machafuko ya kikabila kama yale yaliyoshuhudiwa katika miaka ya 1993-2006.
Vyombo vya sheria vya Burundi viliwahukumu hivi karibuni kifungo cha maisha jela wafuasi 21 wa chama cha upinzani cha MSD kwa kuwatuhumu kwamba “walianzisha vurugu wakitumia silaha”, baada ya makabiliano na polisi ambayo iliwakatila wasifanye mazowezi ya kukimbia, wakati vijana wa chama tawala wamekua wakifanya mazoezi hayo kila jumamosi.


Mkasi - SO8E13 With AY

Friday, March 7, 2014

MTOTO WA GADDAFI,SAADI ASHIKILIWA LIBYA


Serikali ya Libya imesema kuwa mtoto wa Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Saadi Gaddafi, ameondoshwa nchini Niger hivi sasa anashikiliwa mjini Tripoli.
Saadi alitoroka baada ya baba yake, Kanali Muammar Gaddafi kuuawa wakati wa mapinduzi yaliyofanyika mwaka 2011 nchini Libya.
Anashutumiwa kuwafyatulia risasi waandamanaji na anadaiwa kutekeleza uhalifu mwingine wakati wa utawala wa baba yake, yeye alipokuwa Kiongozi wa vikosi maalum vya kijeshi.
Serikali ya Libya imetoa taarifa hiyo mapema siku ya alhamisi kuwa wamempokea akitokea Niger.

awali , Niger ilikataa ombi la Libya ilipotaka imsafirishe Saadi, huku waziri wa sheria wa Niger akihofu kuwa Saadi atahukumiwa adhabu ya kifo.

MALARIA YAWA UGONJWA HATARI ZAIDI

Watafiti kutoka Uingereza na Marekani wanasema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakazua ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kote duniani huku ugonjwa huo ukienea katika maeneo ya milimani barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Katika matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida la Science, wanasayansi hao wanasema hata ongezeko dogo katika viwango vya joto siku za usoni huenda likaongeza kwa mamilioni maambukizi ya malaria.

Mbu anayesababisha malaria.
Watafiti wamepata ushahidi kwamba mbu anayebeba kimelea kinachosababisha malaria wanaelekea katika nyanda za juu wakati viwango vya joto vikipanda.
Watu wanaoishi katika maeneo ya nyanda za juu wanakosa kinga na hivyo kurahisisha maradhi ya malaria kuenea.
Takriban watu milioni mia mbili ishirini kote duniani huambukizwa ukonjwa wa malaria.


Mbu aneyesababisha malaria

Thursday, March 6, 2014

Mkasi - SO8E08 With Inspector Haroun

FOLENI KUBWA MBAGALA MZINGA DARAJANI JANA




Jana Jioni majira ya saa kumi na mbili jioni nilikuwa naelekea maeneo ya Mbagala Kongowe nikakutana na foleni kubwa sana ambayo ilisababishwa na ubovu wa barabara pamoja na magari kutofuata taratibu na sheria barabarani.nilikuwa kwenye bodaboda lakini ilinichuku kama dk 15 hivi kupita kwenye daraja hili kwa jinsi magari yalivyokaa vibaya na kusababisha kufunga njia.
Angalia baadhi ya picha nilizochukua nikiwa kwenye eneo hilo.

hakuna pa kutokea

Hizi ni baadhi ya bodaboda zikiwa kwenye foleni


Monday, January 27, 2014

NGUZO ZA UMEME ZAANGUKA KATIKATI YA BARABARA MAENEO YA BANDARI MWEMBEYANGA



BONANZA MITAANI



Siku ya jana jumapili kulikuwa na matukio mbalimali katika maeneo mengi ya nchi hii,angalia sehemu ya matukio hayo ambayo nilikutana nayo mbagala zakhem katika viwanja vya mpira

wahamasishaji wa moja ya timu zilizokuwa zikishiriki bonanza hilo





Friday, January 10, 2014

Yaya Toure bingwa wa Afrika

Mchezaji wa Manchester City ambaye pia hucheza nafasi ya kiungo cha kati katika timu ya Ivory Coast, Yaya Toure ndiye mwanasoka bora zaidi mwaka 2013 barani Afrika

Toure alikabidhiwa tuzo la (caf) mwaka wa tatu mfululizo katika sherehe zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria Alhamisi usiku.

Taarifa zinazohusianaMichezoAidha Toure pia alishinda tuzo la BBC la mwanasoka bora zaidi barani Afrika mwaka jana.

Alikuwa anawania tuzo hilo dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast Didier Drogba, ambaye huchezea Galatasaray na John Mikel Obi mnigeria ambaye husakata soka nchini Uingereza.

"nimefurahi sana kwa sababu hii ni ishara kuwa nacheza vyema sana ,'' alisema Toure baada ya kupokea tuzo yake.

Lakini alisema kuwa majaji walikuwa na wakati mgumu kumchagua mchezaji bora kwa sababu washindani wenzake wote ni wazuri.

''Sikudhani kama nitashinda kwa sababu Drogba na Obi Mikel ni wasakataji wazuri wa kabumbu,'' aliongeza Toure.


Washidi wa hivi karibuni wa tuzo ya Caf

2013 Yaya Toure
2012 Yaya Toure
2011 Yaya Toure
2010 Samuel Eto'o
2009 Didier Drogba
2008 Emmanuel Adebayor
2007 Frederic Kanoute
2006 Didier Drogba

Abedi Pele wa Ghana alishinda tuzo hiyo mara tatu kati ya mwaka 1991-93 huku Samuel Eto'o akishinda kati ya mwaka 2003-05.

Bila shaka klabu ya Man City anakosakatia kambumbu Toure, bado haishinda kombe lolote la klabu lakini nyota yake imekuwa iking'aa sana nyumbani na katika nyanja za kimataifa.

Toure ndiye mchezaji pekee wa kiafrika kuwa katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwania tuzo la mchezaji bora la FIFA mwaka jana.

Mshindani wake wa karibu aliyekuwa pia anawania tuzo la Caf, Mikel, mwenye umri wa miaka 26, alisaidia Nigeria kushinda kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.
Taarifa zinazohusiana

Kenya:Al shabaab yapata kipigo

Jeshi la Kenya linalopambana na kundi la wanamgambo la al-Shabaab linasema angalau wapiganaji 30 wa kundi hilo wameuawa Kusini Magharibi mwa Somalia.
Msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir ameelezea kuwa jeshi la Kenya lilishambulia kwa mabomu mojawapo ya kambi za kundi hilo katika eneo la Gedo , Alhamisi Jioni.
Aliongeza kwamba miongoni mwa waliofariki ni makamanda kadhaa wa kundi hilo.
Al Shabaab hata hivyo hawajatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Kadhalika Al Shabaab walikiri kufanya shambulizi la kigaidi mjini Nairobi mwaka jana dhidi ya jengo la kifahari la Westgate na kuwaua watu 70.
Kenya imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi hilo tangu mwaka 2011 Oktoba wanajeshi wake walipojiunga rasmi na vikosi vya muungano wa Afrika ambavyo tayari vilikuwa nchini Somalia kwa kazi hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa majeshi ya Kenya yataendelea va vita dhidi ya wanamgambao hao tangu waliposhambulia Kenya mwaka jana.

Mkasi - SO8E01 With Mchungaji Lusekelo

Wednesday, December 18, 2013

Kansiime Anne Profile: Get to know the real me

12 MAHAKAMANI KWA UKEKETAJI SAME

Wanawake 12 ambao ni wazazi wa wasichana 21 waliofanyiwa ukeketaji wilayani Same, mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa Tanzania, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Same, wakati waliposomewa mashitaka yao kwa mara ya kwanza tangu wakamatwe mwishoni mwa wiki iliyopita.
Watuhumiwa wote wanashitakiwa kwa kosa la Ukatili dhidi ya watoto na kuwasababisha maumivu makali, shitaka ambalo wote wamekana.
Tisa kati ya watuhumiwa hao 12 wameachiliwa kwa dhamana, huku watatu wakibaki mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni shilingi milioni mbili za Tanzania, sawa na dola 1250 za Kimarekani.
Miongoni mwa washitakiwa, mmoja alikabiliwa na mashitaka mawili, moja akiwa mzazi wa mmoja wa wasichana waliokeketwa na pia akiwa ngariba.
Kutokana na mila na desturi ya baadhi ya makabila nchini Tanzania, ukeketaji unafanyika japo ni kinyume cha sheria, huku watu wanaokamatwa kuhusika na ukeketaji wakichukuliwa hatua za kisheria.
Kama watapatikana na hatia, wanawake hao wanakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka mitano jela au kutozwa faini kubwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30 Desemba 2013, wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.


Habari kwa hisani ya BBC Swahili

Waliokufa Sudan Kusini ni '400 - 500'


Mamia ya watu wanaaminika kufa wakati wa mapigano baina ya majeshi ya yanayomuunga mkono rais wa Sudan Kusini na yale yanayomuunga mkono makamu wa rais, maafisa wa Umoja wa Mataifa waliopo Sudan Kusini wamesema baada ya kunukuu ripoti ambayo bado haijathibitishwa..
Wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa wamesema wameambiwa na vyanzo vya habari katika mji wa Juba kwamba idadi ya watu waliokufa wanaweza kufikia 400 hadi 500.
Sudan Kusini imekuwa na mapigano ya siku mbili kufuatia taarifa kwamba kulikuwa na jaribio la kumpindua rais Salva Kiir.
Mwanasiasa wa upinzani aliyeko uhamishoni Riek Machar amekana madai ya serikali kuwa alijaribu kufanya jaribio hilo.
"Kilichotokea Juba ni kutokuelewana na mgawanyiko baina ya vikosi vya ulinzi vya rais, sio jaribio la mapinduzi," aliiambia Sudan Tribuni, tovuti yenye makao yake Paris katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya jumatano.
Bwana Machar Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Kusini ambaye aliondolewa na rais Kiir mwezi Julai, amesema hana taarifa wala hausiki kwa namna yoyote na jaribio hilo la mapinduzi.
Rais wa Sudan Kusin Salva Kiir amesema kundi la wanajeshi wanaomuunga mkono makamu wa rais Machar walikuwa wakijaribu kujitwalia madaraka kwa kwa nguvu siku ya Jumapilil usiku, lakini walishindwa.
Wakati mapigano yanaendelea siku ya jumatatu na jumanne, serikali imesema wanasiasa kumi maarufu akiwemo waziri wa zamani wa fedha, wametiwa mbaroni.
Taarifa za mapigano hayo zimefika kwenye baraza la kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya jumanne, ambapo limesema mapigano hayo yanaweza kuwa mapingano ya kikabila.


Mkasi - SO7E11 With Muumin Mwinjuma

Monday, October 28, 2013

Kansiime Anne ready to take on husband number

Mourinho amsifia Torres kwa kuipa Cheslea bao la ushindi

Kocha wa klabu ya soka ya Chelsea nchini Uingereza Jose Mourinho amemsifu mshambulizi Fernando Torres baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Manchester City katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini humo mwishoni mwa juma lililopita

Mkasi - SO7E03 With Lulu

Thursday, October 10, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MBEYA KWA UMMA-AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHIKwa

MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA RELINI – MLOWO  BARABARA YA  MLOWO/KAMSAMBA  WILAYA YA  MBOZIMKOA WA MBEYA. GARI T.353 APR AINA YA  TOYOTA HILUX P/UP  LIKIENDESHWA NA DEREVA  ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA  MTOTO PETRO S/O KAUNDA, MIAKA 3,  KYUSA, PIA MAJERUHI KWA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO AITWAE FAUSTA D/O MBUBA, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITEMPULA AMBAYE AMELAZWA ZAHANATI YA NAZARETH – MLOWO. CHANZO KINACHUNGUZWA.

DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA  KATIKA ZAHANATI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA  MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA  USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA  RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE  KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,  VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

WILAYA YA  KYELA  – KUPATIKANA NA BHANGI. MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA MBUGANI WILAYA YA  KYELA  MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRANK S/O ARON, MIAKA 27,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBUGANI   AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 20 SAWA NA UZITO WA GRAM 120. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE  MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA  ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

 [DIWANI ATHUMANI - ACP]KANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KWA HISANI YA:mbeyayetu.blogspot.com