Serikali ya Urusi imetoa nyaraka kwa Mfanyakazi wa zamani wa
Shirika la Kijasusi nchini Marekani CIA Edward Snowden zinazomruhusu kuondoka
katika eneo la Uwanja Ndege ambalo amekuwa akiishi tangu awasili akitoke China.
Shirika
la Habari la Umma la Urusi RIA limethibitisha kupatiwa kwa nyaraka hizo kwa
Snowden ambaye amekuwa akihaha kuomba hifadhi kipindi hiki akisakwa kwa udi na
uvumba na Serikali ya Marekani baada ya kuvujisha siri za Shirika la CIA.
Nyaraka
hizo zimetoa nafasi kwa Snowden kuweza kuingia nchini Urusi na kuomba hifadhi
ay hata kuondoka na kueleka katika nchi yoyote ambayo itakuwa tayari kumhifadhi
bila ya walinzi wa mpaka kumzuia.
Taarifa
zinasema baada ya Snowden kupatiwa nyaraka hizo muhimu anatazamia wakati wowote
ataondoka katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Moscow alipokuwa anahifadhiwa
sehemu ya abiria wanaopita nchi hiyo kueleka mataifa mengine.
Snowden
amepata nyaraka hizo muhimu kutoka kwa usaidizi wa Mwanasheria wake Anatoly
Kucherena ambaye amekwenda katika Uwanja wa Ndega wa Sheremetyevo kukutana na
mteja wake.
Nyaraka
hizo amekabidhiwa Kucherena ambaye ndiye atamkabidhi Snowden anayetajwa tayari
ameshabadilishiwa hadi mavazi yake tayari kwa kuingia nchini Urusi na kuendelea
na mchakato wa kuomba hifadhi ya kudumu.
Mwanasheria
wa Snowden, Kucherena amesema iwapo mteja wake atakuwa tayari kupatiwa uraia wa
Urusi atafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha anapata nafasi hiyo ambayo
huenda ikatolewa kwake bila pingamizi.
Mapema
mwezi huu Snowden alijitokeza na kuomba hifadhi nchini Urusi ambapo aliambiwa
mchakato wa yeye kupewa hadhi huyo huenda ungechukua hata kipindi cha miezi
mitatu kabla ya kukubaliwa.
Mfanyakazi
huyo wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Nchini Marekani CIA Edward Snowden
amekuwa akippata hifadhi ya muda nchini Urusi kitu ambacho kimechangia kuleta
mgogoro wa uhusiano baina ya Serikali za Washington na Moscow.
No comments:
Post a Comment