Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, kupitia chama chake ODM
wametia saini makubaliano ya kuunda muungano wa kisiasa na Makamo wa Rais
Kalonzo Musyoka ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo wa Machi
mwakani.
Huu utakuwa muungano wa pili kabla ya tarehe ya mwisho (04-12-2012)
iliyowekwa na msajiri wa vyama vya siasa iliyotaka vyama hivyo viwe
vimekamilisha taratibu za kisheria za muungano wa vya muungano wao katika siku
tisini.Hii ni baada ya kushuhudia muungano mwingine kati ya Uhuru Kenyatta na William Ruto mapema wiki hii.Tuesday, December 4, 2012
KILIMANJARO STARTS YAWASUBIRI MSHINDI KATI YA UGANDA NA ETHIOPIA
Tanzania Bara(Kilimanjaro Stars)inamsubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia ambao wanakipiga leo(06-12-2012).
Kilimanjaro stars ilifuzu kuingia nusu fainali jana baada ya kuigalagaza Rwanda kwa mabao 2-0,Mabao ya Amri Kiemba dakika ya 33 na John Bocco dakika ya 53 ndiyo yaliyoifanya Kilimanjaro Stars itinge nusu fainali

BASI LATEKWA
Basi lilikuwa likisafiri kuelekea jijini Mwanza,lilitekwa usiku wa kuamkia juzi maeneo ya Igunga mkoani Tabora katika kijiji cha Igogo.
Basi hilo la Muro lilikuwa likielekea jijini Mwanza lilipofika maeneo ya kikiji cha Igogo kilometa 13 kutoka Igunga mjini lilikutana na mawe yakiwa yamepangwa barabarani na kuwazuia wasiendelee na safari na ndipo kundi la watu wanaokadiriwa kufikia 15 walipovamia na kuwaamuru abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo kutoa simu na fedha walizokuwa nazo na hatimaye kuwavua nguo.
Abiria 3 walijeruhiwa,wakati huohuo Jeshi la Polisi limejipanga kufanya msako mkali ili kuwakamata waporaji hao

Monday, December 3, 2012
TANZANIA YATOKA KIDEDEA MBELE YA RWANDA
Kilimanjaro stars imetoka kifua mbele baada ya kuifunga Rwanda 2-0 katika uwanja wa Kagogo nchini Uganda
PAPA KUANZA KUTUMIA MTANDAO WA TWITTER
Papa Benedict anafungua akaunti
katika mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa
kanisa katoliki.
Taarifa kuhusu akaunti hiyo
itatolewa baadaye hii leo katika mkutano na waandishi habari, lakini habari
kutoka Vatican zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe kwenye akaunti hiyo.
Wanasema Papa Benedict anapendelea
kuandika kwa mkono kuliko kutumia tarakilishi.
Kanisa hilo la katoliki tayari
linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu
unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.
Wakatoliki kote duniani, wataweza
kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi.
MISRI KUPIGA KURA YA MAONI DESEMBA 15
Rais Mursi wa Misri ameitisha kura ya maoni Desemba 15 kuhusiana
na katiba mpya, kwa matumaini ya kumaliza maandamano baada ya tamko lake la
kujilimbikizia madaraka
Uidhinishaji wa katiba hiyo iliyotayarishwa na baraza ambalo linadhibitiwa
kwa kiasi kikubwa na washirika wake wa makundi ya Kiislamu, utaondoa amri
iliyotolewa Novemba 22 ambayo kwa muda inamkinga Mursi dhidi ya uchunguzi wa
mahakama na kuzusha matamshi ya kuonyesha wasi wasi kutoka kwa mataifa ya
magharibi.Amri hiyo iliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mbaya kabisa kuwahi kutokea tangu pale Mursi aliposhinda katika uchaguzi mwezi Juni na kuzusha maandamano nchi nzima pamoja na ghasia ambamo watu wawili walipoteza maisha na mamia wamejeruhiwa.
UHURU NA RUTO WAUNGANA
Wanasiasa wawili wa Kenya
wanaotaraji kugombea uongozi na ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya
Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa
wanaungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema
atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea
mwenza wa Bwana Kenyatta.
Siku ya Ijumaa shirika la Kenya la
kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha kesi
mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka.
Sunday, December 2, 2012
MISRI WAFANYA MAANDAMANO MAKUBWA BAADA YA MUSWADA WA KATIBA KUIDHINISHWA
Mamia kwa maelfu ya waandamanaji waliingia mitaani mjini Cairo jana Ijumaa kuongeza shinikizo kwa rais Morsi baada ya jopo lenye wajumbe wengi kutoka kundi la Kiislamu kupitisha mswada wa katiba wa nchi hiyo.
Katiba hiyo mpya ambayo imeidhinishwa baada ya vikao virefu usiku wa jana na ambayo imesusiwa na wajumbe wenye msimamo wa kati na Wakristo inazua wasi wasi mkubwa kuhusu masuala ya haki za binadamu,ikiwa ni pamoja na uhuru wa kidini, wanasema wanaharakati.
Rais Morsi atapitia upya mswada huo leo Jumamosi,amesema spika wa bunge Hossam el-Ghiriani, na anatarajiwa baadaye kuitisha kura ya maoni katika muda wa wiki mbili.

Saturday, December 1, 2012
UIGEREZA YASITISHA MISAADA RWANDA
Serikali ya Uingereza imesitisha kwa
muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa
nchi hiyo katika mzozo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mawaziri walisema kwamba Uingereza
sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21.
Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha
pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba, hata baada ya tetesi kwamba ilikuwa
inawaunga mkono wanamgambo wa M23 wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali ya Uingereza ilikuwa
imesema kwamba ingetoa kitita kingine cha pauni milioni 18 kwa ajili ya
mahitaji ya kibandamu ya dharura huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
JIHADHARI KIGOGO MBUYUNI
Maeneo ya Kigogo Mbuyuni limeibuka kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 12-14,linalojiita Panya Road ambalo limekuwa likihatarisha maisha ya wananchi wa maeneo hayo na wapitao maeneo hayo.Kundi hilo ambalo huwa na vijana kati ya 20 na 25 na wanatembea na mapanga na wakikutana na mtu yeyote wanafanya vitendo vya kialifu.Wananchi wa maeneo hayo wamelalamika juu ya kundi hilo.Wakati huohuo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamanda Charles Kenyela ametoa taadhari kwa kundi hilo kwa kuwa sasa watakuwa makini ili kulidhibiti kundi hilo.
ATUMIA MATATU(DALADALA)NCHINI KENYA KUHAMASISHA KUPINGA MAAMBUKIZI YA UKIMWI
Mwathirika wa Virusi vya ukimwi Nchini Kenya anatumia daladala yake kuelemisha watu kujilida dhidi ya maambikizi ya Ukimwi.Bwana Virus kwa jina lake la utani yeye anaishi na virusi vya Ukimwi kwa miaka 9 sasa na amejaaliwa kupata watoto 4,Anashauri watu kupima ukimwi ili kujijua afya yako
Subscribe to:
Posts (Atom)