Papa Benedict anafungua akaunti
katika mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa
kanisa katoliki.
Taarifa kuhusu akaunti hiyo
itatolewa baadaye hii leo katika mkutano na waandishi habari, lakini habari
kutoka Vatican zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe kwenye akaunti hiyo.
Wanasema Papa Benedict anapendelea
kuandika kwa mkono kuliko kutumia tarakilishi.
Kanisa hilo la katoliki tayari
linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu
unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.
Wakatoliki kote duniani, wataweza
kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi.
No comments:
Post a Comment