Saturday, December 1, 2012

UIGEREZA YASITISHA MISAADA RWANDA



Serikali ya Uingereza imesitisha kwa muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa nchi hiyo katika mzozo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mawaziri walisema kwamba Uingereza sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21.
Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba, hata baada ya tetesi kwamba ilikuwa inawaunga mkono wanamgambo wa M23 wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali ya Uingereza ilikuwa imesema kwamba ingetoa kitita kingine cha pauni milioni 18 kwa ajili ya mahitaji ya kibandamu ya dharura huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

No comments:

Post a Comment