Rais Mursi wa Misri ameitisha kura ya maoni Desemba 15 kuhusiana
na katiba mpya, kwa matumaini ya kumaliza maandamano baada ya tamko lake la
kujilimbikizia madaraka
Uidhinishaji wa katiba hiyo iliyotayarishwa na baraza ambalo linadhibitiwa
kwa kiasi kikubwa na washirika wake wa makundi ya Kiislamu, utaondoa amri
iliyotolewa Novemba 22 ambayo kwa muda inamkinga Mursi dhidi ya uchunguzi wa
mahakama na kuzusha matamshi ya kuonyesha wasi wasi kutoka kwa mataifa ya
magharibi.Amri hiyo iliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mbaya kabisa kuwahi kutokea tangu pale Mursi aliposhinda katika uchaguzi mwezi Juni na kuzusha maandamano nchi nzima pamoja na ghasia ambamo watu wawili walipoteza maisha na mamia wamejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment