Wanasiasa wawili wa Kenya
wanaotaraji kugombea uongozi na ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya
Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa
wanaungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema
atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea
mwenza wa Bwana Kenyatta.
Siku ya Ijumaa shirika la Kenya la
kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha kesi
mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka.
No comments:
Post a Comment