Sunday, December 2, 2012

MISRI WAFANYA MAANDAMANO MAKUBWA BAADA YA MUSWADA WA KATIBA KUIDHINISHWA

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji waliingia mitaani mjini Cairo jana Ijumaa kuongeza shinikizo kwa rais Morsi baada ya jopo lenye wajumbe wengi kutoka kundi la Kiislamu kupitisha mswada wa katiba wa nchi hiyo.
Katiba hiyo mpya ambayo imeidhinishwa baada ya vikao virefu usiku wa jana na ambayo imesusiwa na wajumbe wenye msimamo wa kati na Wakristo inazua wasi wasi mkubwa kuhusu masuala ya haki za binadamu,ikiwa ni pamoja na uhuru wa kidini, wanasema wanaharakati.
Rais Morsi atapitia upya mswada huo leo Jumamosi,amesema spika wa bunge Hossam el-Ghiriani, na anatarajiwa baadaye kuitisha kura ya maoni katika muda wa wiki mbili.