![]() |
Abiria wakiwa ndani ya meli hiyo tayari kwa kuanza safari |
![]() |
Meli ya MV Victoria muda wa saa 3.10 ikiwa inaanza safari kuelekea Bukoba |
Meli ya Abiria na Mizigo inayofanya safari zake kati ya jiji
la Mwanza na Bukoba imenusurika kuungua majira ya saa9:15 katika bandari ya Mwanza.Moto
huo ulianza katika meli hiyo baada ya mafundi wa kucholea waliokuwa wakifanya
ukarabati katika meli na cheche kurukia katika madodoro yaliyokuwa katika
sehemu ya mizigo.kikosi cha zimamoto kilifika kayika tukio hilo muda mfupi
baada ya moto kutokea na kufanikiwa kuuzima moto.meli hiyo ilikuwa ikmewasili
kutoka bukoba muda wa asubuhi na ilikuwa inategemewa kufanya safari nyingine
usiku wa leo.
Wafanyakazi wa meli hiyo wamelaani kitendo hivho cha meli
kufanyiwa ukarabati katikatik ya wiki baada ya mwisho wa wiki.Chuma kilichokuwa
kmehifadhi magodoro hayo pamoja na samaki kiliteketea na moto huoambapo mito ya
viti yapatayo 400 yaliteketea kabisa.hasara kamili iliyosababishwa ba noto huo
bado haijafahamika.Habari zinasema licha ya moto huo kutokea lakini meli hiyo ilifanya safari yake kama kawaida kuelekea Bukoba mnamo muda wa saa 3.10 usiku
No comments:
Post a Comment