JENGO la Makao Makuu ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) liko
hatarini kupigwa mnada kwa amri ya Mahakama kutokana na kushindwa kulipa
deni inalodaiwa na Kampuni ya Huduma za Utalii ya Leisure Tours and
Holidays.
Tayari Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru
kampuni hiyo ifanye uthamini wa jengo hilo na kuwasilisha mahakamani
taarifa hiyo leo.
Hatua hiyo inatokana na mao mbi yaliyowasilishwa
mahakamani hapo na kampuni hiyo ambayo ni mshindi wa tuzo katika kesi ya
madai namba 56 ya mwaka 2009 iliyotokana na mgogoro wa kibiashara baina
yake na ATCL.
Kampuni hiyo inaidai ATCL Dola za Marekani
716,259.25 (Sh1.1 bilioni) baada ya kushindwa kulipia huduma za
ukodishaji wa magari ambazo kampuni hiyo ilitoa kwa ATCL.
Mbali na kiasi hicho ambacho ni deni la msingi
pamoja na riba ya asilimia 10 kwa kipindi cha miaka miwili, pia ATCL
inapaswa kuilipa kampuni hiyo gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
Katika amri ya Mahakama hiyo iliyotolewa na Jaji Mfawidhi Robert Makaramba Februari 11, 2013, kabla ya kutoa amri ya jengo hilo kupigwa mnada, ilimwamuru mshinda tuzo kufanya uthamini wake.
Katika amri ya Mahakama hiyo iliyotolewa na Jaji Mfawidhi Robert Makaramba Februari 11, 2013, kabla ya kutoa amri ya jengo hilo kupigwa mnada, ilimwamuru mshinda tuzo kufanya uthamini wake.
Taarifa ya amri hiyo inasomeka: “Amri:
Muombaji/mshinda tuzo anatakiwa kuwasilisha katika Mahakama hii taarifa
ya uthamini wa jengo la ATCL, lililoko katika Mtaa wa Ohio, (Dar es
Salaam) saa 3.00 asubuhi, Februari 20, 2013. Shauri litakuja kwa amri
zaidi saa 3.00 asubuhi, Februari 25, 2013,” inasomeka amri hiyo.
Hata hivyo, Wakili wa mshinda tuzo, Jerome Msemwa
wa Kampuni ya Msemwa & Company Advocates, alisema licha ya amri ya
Mahakama kufanya uthamini wa jengo hilo, lakini maofisa wa mshindwa tuzo
wamezuia kufanyika uthamini.
Wakili Msemwa alisema maofisa hao wa mshindwa tuzo walizuia uthamini huo kufanyika kwa madai kuwa watalipa.
Wakili Msemwa alisema maofisa hao wa mshindwa tuzo walizuia uthamini huo kufanyika kwa madai kuwa watalipa.
Alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiahidi
hivyo bila utekelezaji na kwamba leo anawasilisha mahakamani taarifa
hiyo ya kuzuiwa na kisha kusubiri amri ya Mahakama.
Awali, Novemba 20, 2012, Mahakama hiyo ilimwamuru mshindwa tuzo kuwasilisha mahakamani hapo jedwali la malipo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe ya amri hiyo.
Awali, Novemba 20, 2012, Mahakama hiyo ilimwamuru mshindwa tuzo kuwasilisha mahakamani hapo jedwali la malipo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe ya amri hiyo.
Hata hivyo, mshindwa tuzo hakutekeleza amri hiyo ndipo mshinda tuzo alipowasilisha maombi ya kukamata na kuuza jengo hilo.
Katika kesi ya msingi pande zote zilikubaliana
kuzungumza na kufikia mwafaka nje ya Mahakama, makubaliano ambayo kila
upande ulisaini ikiwa ni ishara ya kukubali kutekeleza.
Waliwasilisha mahakamani makubaliano hayo, Aprili 8, 2011 ili yaidhinishwe na kuwa uamuzi halali.
Waliwasilisha mahakamani makubaliano hayo, Aprili 8, 2011 ili yaidhinishwe na kuwa uamuzi halali.
Katika makubaliano hayo, mshindwa tuzo anapaswa
kumlipa mshinda tuzo kiasi cha Dola 596,882.97(Sh952 milioni) kwa awamu
tatu za kiasi cha Dola 198,960.99 (Sh317 milioni) kwa kadri anavyopata
fungu kutoka Hazina.
Pia, walikubaliana mshindwa tuzo amlipe mshinda
tuzo kiasi cha Dola 119, 376.97(Sh190 milioni) kikiwa ni riba ya
asilimia 10 kwa mwaka ya malipo ya msingi, kwa kipindi cha mwaka wa 2009
na 2010, kwa awamu tatu kadri anavyopata fungu kutoka Hazina.
Hata hivyo, ATCL haikutekeleza ulipaji wa fidia hiyo kama walivyokubaliana na jinsi Mahakama ilivyoamuru.
source:Mwananchi
Hata hivyo, ATCL haikutekeleza ulipaji wa fidia hiyo kama walivyokubaliana na jinsi Mahakama ilivyoamuru.
source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment