Tuesday, February 12, 2013

SITTA NA LOWASA WATEMWA KAMATI KUU CCM




Makada wa CCM waliotangaza nia ya kugombea Urais katika Chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wametoswa katika nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho CC.
Waliotoswa katika nafasi hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa pamoja na mawaziri wengine walioko madarakani kama  Samuel Sitta (Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Bernard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa).
Mbali na mawaziri hao makada wengine waliotoswa katika uchaguzi huo ni pamoja na January Makamba, Martin Shigela, Willison Mukama, Mohamed Seif Khatib, Omar Yusufu Mzee hata hivyo taarifa za ndani ya NEC ya CCM iliyonaswa na imedai kwamba baadhi ya makada hao wametoswa kutokana kile kinachoelezwa kwamba wanadalili na makundi ndani ya Chama hicho.
Kwa upande wa wale ambao majina yao yalipishwa katika uchaguzi huo lakini wakaangukia pua ni pamoja na Balozi Ali Karume, Gwaride Jabu, Dk Raphael Chegeni, Dk Cyril Chami, Michael Lekule Laizer, Ramadhan Madabida, Hassan Wakasuvi, Dk Fenella Mukangara, Shamsa Mwangunga na Said Mtanda.

No comments:

Post a Comment