Kanisa
Katoliki nchini Ujerumani limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya
kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.
Uamuzi
huu umefanywa kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani
baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa
matibabu siku mbili mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa
Katoloki zikisema kuwa kuzima mimba ni kinyume cha maongozi yake.
Maaskofu
nchini Ujerumani wamekuwa wakijikuta njia panda, ambapo upande mmoja
wanahangaishwa na msimamo wa Kanisa Katoliki, na kwa upande mwingine tatizo
lililompata mwanamke huyo aliyebakwa, kufukuzwa na hospitali zinazosimamiwa na
Kanisa hilo zilizoko mjini Cologne.
Mwishowe
Maaskofu hao walikubaliana kuwa itakuwa halali ikiwa tembe hizo zitatumiwa na
mwanamke aliyebakwa kwa lengo la kuzuia kushika mimba badala ya kutoa mimba
Hii ina
maana kuwa itaweza kutumiwa tu kama kifaa cha kuzuia kushika mimba lakini sio
kuavya. Tembe hizo hutumiwa na wanawake wengi wasiotaka kushika mimba baada ya
tendo la ndoa.
Hata
hivyo Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, ambako Papa wa sasa alitoka,
limegawanyika kufuatia tendo hilo la ubakaji.
Ubishi
kama huo nchini Marekani haukufikia uamuzi baada ya pande zote zilizokuwa
zikibishania dawa hiyo kusema kuwa ni vigumu kujua kama baada ya kitendo cha
ndoa asubuhi inayofuata mwanamke ameshika mimba au la.
No comments:
Post a Comment