Wednesday, February 6, 2013

TAMKO LA CHADEMA

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr.Willbrod Slaa amefanya mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema
1. CHADEMA Inalaani uonevu na uvunjwaji wa Kanuni unaofanywa na kiti cha Spika
2. Hoja zote za CHADEMA zilizokataliwa Bungeni zitapelekwa kwenye mahakama kubwa kuliko zote nayo ni MAHAKAMA YA UMMA
3. Hakuna Mbunge yoyote wa CHADEMA akayeenda kuhojiwa na kamati Uongozi ya maadili ya Bunge mpaka hapo rufaa zote zaidi ya 10 za Wabunge wa CHADEMA dhidi ya maamuzi ya kiti cha Spika zitakapojibiwa
4. Ni aibu kwamba Bunge la sasa halina rejesta ya maamuzi ya Spika kama ilivyo kwa Mabunge mengine ya Jumuiya ya Madola hali inayomfanya Spika na Naibu wake kujiamulia mambo kienyeji tu bila kufuata Kanuni za Bunge na bila kuweka rekodi ya maamuzi yao kwenye hoja mbalimbali.
5. CHADEMA haitakubali dhuluma wala uonevu wowote mwaka huu kwani mwaka huu ni mwaka wa NGUVU YA UMMA

No comments:

Post a Comment