Saturday, February 2, 2013

BARACK OBAMA ATANGAZA MWEZI FEBRUARI KUWA NATIONAL AFRICAN AMERICAN HISTORY MONTH

Rais wa Marekani Barack Obama jana tarehe 31 Januari 2013 ametangaza mwezi wa Februari kuwa mwezi wa kihistoria mwezi wa February utafahamika kama “National African American History Month”. Obama ametaka sekta mbali mbali za kibinafsi na za kiserikali kuchukua mwezi huu na kuandaa vitu ambavyo vitakuwa vinatoa heshima kwa watu ambao wamepita na walipigania usawa kwa watu wote, kuondoa hali ya ubaguzi kati ya mtu na mtu iwe mweupe au mweusi, unaamini dini gani au dini gani wote ni wamoja. Dr. King, President Lincoln na wengine walioitengeneza Marekani na kufanya tujivune, tukiangalia ikiwa ni sehemu ya kibiashara kwa ajili ya watu wote. Mwezi wa Februari utakuwa ni mwezi wa kukumbuka wote waliofanya Marekani kuwa ilipo waliopigania katika sekta zote ilimradi kuleta usawa.

No comments:

Post a Comment