Polisi nchini Afrika Kusini wamewakamata watu
wanaoaminika kuwa washukiwa wa kundi la waasi wa M23 wanaoendeshea
harakati zao katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Polisi wanasema kuwa wamewazuilia katika mkoa wa Lompopo Kaskazini mwa nchi.
Inaarifiwa walikamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi baada ya kupokea habari katika operesheini iliyofanywa kwa miezi kadhaa.
Washukiwa hao, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye leo.
Waasi wa M23 walianza harakati zao, Mashariki
mwa DRC mwaka jana na kwa siku kadhaa kuuteka mji wa Goma , hatua
iliyowalazimisha maelfu ya watu kutoroka makwao na kukimbilia usalama
wao.
No comments:
Post a Comment