Thursday, February 7, 2013

ASKARI AUWAWA AKIWA KAZINI

Askari aliyejulikana kwa jina la Jafari Karume Mohamed ameuwawa kwa kupigwa na risasi na majambazi huko jijini Mbeya.askari huyo aliuwawa akiwa katika mapambano ya kutupiana risasi na majambazi hayo ambayo yalikuwa yametoka kupora kwenye kituo cha mafuta cha Samora Muyombe.Baada ya majibizano ya muda ya risasi majambazi hao walifanikiwa kumjeruhi askari huyo upande wake wa kulia karibu na mbavu na baadae askari huyo alipoteza maisha.Katika tukio hilo jambazi mmoja kwa jina la Shabani Msule 33 mkazi wa Makambako Njombe aliuwawa katika tukio hilo ambaye alikuwa akiendesha gari ambalo lilikuwa likitumiwa na majambazi hao.Majambazi hao walikuwa wakitumia silaha aina ya SMG.walifanikwa kupora kiasi cha Tsh milioni 2 na laki 2.tukio hilo ni la pili kutokea katika jiji hili hivi karibuni.Hii inasemekana ni kwa kuwa wilaya ya Mbozi imekuwa ikiongoza katika matukio ya utengenezaji silha za kienyeji.Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Barakaeli Masaki amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kama watahisi kuna vitendo vya kihalifu .

No comments:

Post a Comment