Monday, January 7, 2013

SUDAN ZAKUBALIANA KUTEKELEZA MAKUBALIANO

Marais wa Sudan na Sudan kusini wamekubaliana jumamosi (05.01.2013)kuhusu muda utakaopangwa kwa ajili ya utekelezaji wa masuala muhimu,wakati walipokutana kwa faragha katika mji mkuu wa Ethiopia ,Addis Ababa.
Usalama, mafuta na mipaka ni miongoni mwa masuala ambayo rais wa Sudan ya kusini Salva Kiir na mwenzake wa Sudan Omar Hassan al - Bashir waliyajadili mjini Addis Ababa kwa upatanishi wa umoja wa Afrika.
Pande hizo mbili zimekubaliana kuwa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika katika mwezi wa septemba mwaka jana yanapaswa kutekelezwa, bila masharti yoyote, amesema mpatanishi wa umoja wa Afrika , rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki. "Jopo letu linatayarisha utaratibu wa utekelezaji wa makubaliano yote yaliyokwisha fikiwa kwa kupanga muda maalum, amesema Mbeki.
Muda utakaopangwa utakamilika ifikapo Januari 13, Mbeki amesema. " Mkutano huo unapaswa kuhakikisha kuwa maamuzi muhimu yanachukuliwa ili kuunda eneo salama ambalo halitakuwa na shughuli za kijeshi," kama ilivyoelezwa katika mkutano wa Septemba.
Katika hatua nyingine , muungano wa vyama vya upinzani pamoja na makundi ya vyama vya kijamii umetia saini makubaliano siku ya Jumamosi (05.01.2013) mjini Khartoum ukitoa wito wa kuangushwa kwa utawala wa Sudan na kufanya uchaguzi huru na wa haki.
Makubaliano hayo , yaliyopewa jina la "Mapambazuko mapya, " yanalenga katika kuleta suluhisho kwa uchumi wa Sudan pamoja na mzozo wa kisiasa , elimu na afya.

No comments:

Post a Comment