Friday, January 18, 2013

MILLARD AYO AOMBA DUWA ZENU KUKABILIANA NA VITA YA WA MASAI NA WASONJO HUKO LOLIONDO

Millad Ayo akiwa ndani ya gari ya askari kuanza safari
Kijana mdogo mwenye sauti ya bass ambeye anapiga mzigo pale clous redio sasa yupo huko loliondo kupata story ya babu wa loliondo ila mara baada ya kufika huko amepata taarifa kuwa kuna vita kali kati ya wamasai na wasonjo huku silaha zinazotumika ni mishale na na bunduki sasa yupo katika wakati mgumu anaomba duwa zenu kama alivyoandika.katika kurasa yake.

Good morning watu wangu, nimefika Loliondo salama, kazi imebaki kushuka kwa babu sasa ila nimeshtushwa kusikia sasa hivi kuna vita kubwa ya risasi na mishale ya Wamasai na Wasonjo, na ninakokwenda ndio wanapigana, kiukweli siwezi kuiacha hii stori ya babu, naondoka na gari ya polisi, maombi yenu muhimu.

Source:THE SUPER STARS

No comments:

Post a Comment