Mashambulizi wa Swanse Michu, amesaini mkataba mpya, na kuongeza muda wake na klabu hiyo kwa muda wa miaka minne ijayo.
Mchezaji huyo kutoka Uhispania, ameibuka kuwa
miongoni mwa wachezaji bora wa ligi kuu ya Premier ya England tangu
aliposajiliwa kwa kitita cha pauni milioni mbili nukta mbili na klabu ya
Rayo Vallecano.
Michu mwenye umri wa miaka 26, sasa atasalia katika klabu hiyo hadi mwaka wa 2016.
Akiongea baada ya kusaini mkataba huo, Michu alisema, hakuwa na ugumu wowote kuongeza muda wake na Swanse.
Nyota huyo ambaye ana uwezo wa kucheza kama
mcheza kiungo au mshambuliaji, amefunga magoli 16 baada ya kucheza mechi
ishirini na nane.
Wachambuzi wa masuala ya soka nchini England
wanasema kuwa kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi
kusajiliwa na klabu hiyo ya Swansea.
Kocha wa Swansea, Michael Laudrup, amemsifu
mchezaji huyo kwa mchango wake katika ufanisi wa klabu hiyo na kumtaja
kama kito ya msimu.
No comments:
Post a Comment